Konda akikuuliza una mia hapo huwaga unampa au ...?

Konda akikuuliza una mia hapo huwaga unampa au ...?

konda huwa unampaga ile shilingi mia ..?

  • NAVUNGA TU

  • nampatia kiroho safi


Results are only viewable after voting.
Mimi ruti yangu nauli ni 600 ila kila siku nalipa 500. Ila nahakikisha nina 500 kavu.
Kuna muda makonda huwa wanakuwa hawana chenji kwahiyo unakuta abiria wote tunakatwa 500 gari linapokaribia kituoni.

Konda anaona ni heri mfaidike ninyi abiria kuliko aombe chenji kwa wale jamaa wa vituoni wanaķata 200 kwa kila 1000.
 
Nikiwa nayo nampatia katika vitu sipendi ni ubishi wa ajabu ajabu na makonda, au mtu yeyote lakini mada inasema ni konda so nampatia

Nishawahi kuwa na nauli pungufu na ninapotoka kwenda ni mbali nikamwomba kiroho safi akakubali....

@Dr Am 4real PHD
 
Back
Top Bottom