Konde (Harmonize) acha kutumia "sembe" inakuharibia career yako ya muziki

Konde (Harmonize) acha kutumia "sembe" inakuharibia career yako ya muziki

sinza pazuri

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
3,344
Reaction score
9,066
Kwa mapenzi mema namshauri Konde boy aache kutumia poda, ajifunze kwa kaka zake waliopotea kwa kuendekeza poda.

Management yake msimuogope boss wenu msaidieni kabla gari haijawaka, ikiwaka hakuna sober house itayomsaidia. Haya mengine mengi mnayoyasikia ni matokeo ya stress na kuchanganywa na unga.


------------------------

Kila jambo linataratibu zake msanii Harmonize asipobadilika anaelekea kujiharibia ktk tasnia yake ya muziki.

Wito kwa watu wake wakaribu wamshauri jinsi gani ya kutumia mitandao ya kijamii na jinsi gani ya kutengeneza kiki sababu kila uchwao anelekea kudrop katika fani, Harmo wa WCB sio huyu wa sasa kashfa nyingi,kazi hazina ubora ,michambo na mabifu na watu kila kukicha.

Tahadhari kwa sisi mashabiki wake tunaona mwisho mbaya kwake anatakiwa apate washauri na wasimamizi watakaomshauri na kumuelekeza nini afanye nini aache kulinda weledi wa tasnia yake.

Watanzania hawakawii kumchoka mtu mifano hai ipo mingi kwa wasanii wenzake, anatakiwa akumbuke alipotoka na aangalie alipo na anapokwenda.

Kikawaida katika nchi yenye kulinda tamaduni na ustaarabu ktk jamii kitendo cha kuonesha picha za utupu mitandaon ni cha fedhea kwa msanii mkubwa Kama yeye.

Kitendo cha kula kuku na mayai yake ni kudhalilisha wanawake na hakivumiliki, kitendo cha kutukana watangazaji na kuwapa vitisho kama alivyomfanyia Maimartha wa Jesse ni ulimbukeni na upungufu wamaarifa, kitendo cha kutengeneza lebo ya kusimamia wasanii halafu wasanii hao hawatoi nyimbo wala hawasikiki na wanavipaji ni kuua vipaji vya wasanii wetu.

Mimi shabiki namba moja wa Harmonize na nimechukizwa na mienendo yake, naomba abadilike bado tunampenda kushindana na WCB kutamuharibia wale watu hawawezekaniki wana nguvu na vipaji na washapiga hatua kubwa Sana .
 
Back
Top Bottom