Habari za Zanzibar
New Member
- Dec 18, 2024
- 4
- 2
Ubalozi wa Saudi Arabia kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Kituo cha Kuendeleza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) wameandaa na kushiriki Kongamano la Biashara na Uwekezaji, lililofanyika Katika Ukumbi wa Makao makuu ya Chemba ya Riyadh yaani (the international conversation and exhibition Centre ) Saudi Arabia lililoanza mapema 17 Desemba na kutarajiwa kukamilika 21 Desemba, 2024.
Kongamano hili limehudhuriwa na Mawaziri mbalimbali wa kisekta, wakiwemo Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye ni mmoja wa viongozi walioshiriki katika jukwaa hilo.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano hili alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, ambaye alieleza kuwa licha ya ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Saudi Arabia kudumu kwa zaidi ya miaka 40, kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kimekuwa kidogo.
Mhe. Prof. Kitila Mkumbo alibainisha kuwa, kwa upande wa Saudi Arabia, mauzo ya nje nchini Tanzania yamefikia dola bilioni 52.3, wakati mauzo ya Tanzania kwa Saudi Arabia yamefikia dola milioni 12.3 pekee.
Alisisitiza kuwa, kwa kuzingatia fursa kubwa za kiuchumi na mazingira bora ya uwekezaji yaliyopo nchini Tanzania, ni wakati muafaka kwa kampuni za Saudi Arabia kushirikiana na wenzao wa Tanzania kuongeza uwekezaji na biashara, hasa katika sekta za kilimo, usindikaji bidhaa za kilimo, nishati ya kijani, uchumi wa buluu, madini, mafuta na gesi, pamoja na masuala ya kidijitali.
Jukwaa hili linalenga kukuza ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Saudi Arabia, huku likilenga kuvutia mitaji, kuongeza biashara na kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi hizo mbili. Hii ni hatua muhimu ya kuelekea kwa maendeleo endelevu kupitia ushirikiano wa kimataifa na uwekezaji wa pande zote.

Attachments
-
IMG-20241223-WA0350.jpg177.4 KB · Views: 4 -
IMG-20241223-WA0349.jpg191.4 KB · Views: 3 -
IMG-20241223-WA0345.jpg165.5 KB · Views: 4 -
IMG-20241223-WA0345(1).jpg165.5 KB · Views: 2 -
IMG-20241223-WA0351.jpg143.7 KB · Views: 1 -
IMG-20241223-WA0354.jpg192.1 KB · Views: 5 -
IMG-20241223-WA0353.jpg231.2 KB · Views: 2 -
IMG-20241223-WA0352(1).jpg253.3 KB · Views: 2 -
IMG-20241223-WA0352.jpg253.3 KB · Views: 1 -
IMG-20241223-WA0342.jpg202.9 KB · Views: 3 -
IMG-20241223-WA0343.jpg217.9 KB · Views: 3 -
IMG-20241223-WA0344.jpg202.5 KB · Views: 1 -
IMG-20241223-WA0341.jpg218.4 KB · Views: 2 -
IMG-20241223-WA0337.jpg195.4 KB · Views: 2 -
IMG-20241223-WA0338.jpg188.7 KB · Views: 3 -
IMG-20241223-WA0340.jpg165.9 KB · Views: 1 -
IMG-20241223-WA0357.jpg157.6 KB · Views: 1 -
IMG-20241223-WA0356.jpg178.7 KB · Views: 2 -
IMG-20241223-WA0355.jpg188.1 KB · Views: 2 -
IMG-20241223-WA0348.jpg201.7 KB · Views: 3 -
IMG-20241223-WA0359.jpg231 KB · Views: 1