Kongamano la Katiba mpya lafanyika Tarime kwa amani na utulivu

Kongamano la Katiba mpya lafanyika Tarime kwa amani na utulivu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Siku zote tumesema humu na kurudia mara nyingi sana kwamba , HAKUNA MAHALI POPOTE KATIKA DUNIA HII AMBAPO SHETANI ALIWAHI KUMSHINDA MUNGU , japo wapagani wametupuuza mara zote lakini ukweli huu hauwezi kupingwa .

Pamoja na RC wa Mara kumwaga majeshi yote barabarani na mitaani , ikiwa ni pamoja na kulinda ofisi ya Chadema Musoma Mjini kwa masaa yote, lakini Kongamano la Katiba Mpya limefana kupita maelezo huko Tarime , halafu hakuna amani yoyote iliyotoweka , ilikuwa mada juu ya mada , hawa wanaosema kongamano linavuruga amani ni WAONGO.

Ushahidi huu hapa

FB_IMG_1630783806256.jpg
FB_IMG_1630783813373.jpg
FB_IMG_1630783820884.jpg
 
Safi Chadema ndio inatakiwa iwe hivyo,mtu mwenye akili ndogo ni wa kuzungushwa tu maana hana uwezo wa kushindana na akili kubwa

Sasa tuwaulize intelijensia ya Polisi ambayo huwa wanaisema leo illikuwa wapi?
 
Katiba mpya mliikataa nyie wenyewe Chadema mkiongozwa na Mbowe akajifanya kuunda Ukawa. Leo mnatafuta bahati mliyochezea!

Tambueni lila jambo na wakati wake. Katiba mpya siyo ajenda yetu sisi wananchi kwa wakati huu.
 
Siku zote tumesema humu na kurudia mara nyingi sana kwamba , HAKUNA MAHALI POPOTE KATIKA DUNIA HII AMBAPO SHETANI ALIWAHI KUMSHINDA MUNGU , japo wapagani wametupuuza mara zote lakini ukweli huu hauwezi kupingwa .
Kwani CCM in "wapagani"?
 
Back
Top Bottom