Didia
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 719
- 260
Katika kongamano lililoisha juzi UDSM mada kuu iligusa maeneo makuu matatu: Haja, Mchakato na Maudhui ya Katiba Mpya. Wajumbe wote walionekana kukubalina hususani na kipengele cha kwanza-Haja ambapo kila mtu alionesha kuwepo umuhimu wa kupata katiba mpya. Hivyo hapo hakuna mjadala zaidi.
Katika kipengele cha pili kinachozungumzia mchakato yaani katiba ipatikane kupitia njia/utaratibu upi mpaka sasa kuna hoja tatu zinazokinzana. Napenda nizipe majina yafuatayo:
1. Hoja ya Rais: Rais kuunda tume ikusanye maoni na kutoa ushauri ambao utashugulikiwa na vyombo vya kikatiba. Maoni ya wajumbe yalionesha kuwa kauli ya Rais haiko wazi na wengi wanaamini kuwa utaratibu wa tume ya Rais hautaleta matunda yenye kutarajiwa kama historia inavyoonesha.
2. Hoja ya Mnyika: Kupeleka Hoja Binafsi Bungeni, yafanyike marekebisho ya katiba kuingiza ibara itakayo toa muongozo jinsi ya kutunga katiba mpya. Itungwe sheria inayo unda chombo cha kuratibu maoni ya wananchi......
3. Hoja ya Shivji (tunaweza kuiita pia mtazamo wa Asasi za Kiraia): Tume ya Rais isimamie mchakato wa kukusanya maoni, iwe wazi, isiripoti kwa Rais bali kwa wananchi.
Hoja iliyotolewa na Shivji ni kwamba Mnyika akipeleka hoja ya katiba bungeni matokeo yake huenda yasiwe mazuri ikizingatiwa wingi wa wabunge wa CCM. Mtazamo huu unaimanisha kuwa hoja ya katiba ikionekana kuwa himaya ya chama fulani patakuwepo mgawanyiko kati ya wananchi/wadau na huenda pasiwepo msukumo wa kutosha. Mapendezo yaliyotolewa ni kwamba nguvu sasa ihamie (i) kusukuma Rais aunde tume ambayo haita ripoti kwake, bali kwa wananchi. (ii) Katiba isiandikwe na Mwanasheria Mkuu bali wajumbe watakao teuliwa na bunge la mda (Constituency Assembly)
Je, kuna haja ya Mh. Mnyika kuendeleza mchakato wa hoja binafsi? Nini itakuwa athari au faida za kupeleka hoja binafsi bungeni? Je kama unakubalina na hoja za Shivji ni mikakati gani tufanye kufanikisha hilo?

- Kwakuwa swala lamaudhui (yaani tuwe na katiba ya namna gani ni pana sana, naomba mjadala ujikite zaidi kwenye mchakato i.e njia ipi itumike kupata katiba mpya)