katika hali ya kushitua na kushangaza,kesho wakati UDSM wakiwa wameamua kuwa na kongamano kubwa la kujadili uwepo wa katiba mpya,lipo kundi la watu ambao wanadai kuwa ni waislamu na wao wameamua kuitisha kongamano lao kesho ktk ukumbi wa karimjee na wanategemea kutoa matamko mbalimbali lengo ni kuhakikisha kuwa media itaondoa attention kwenye katiba. pia watatoa matamko controversial sana juu ya utawala kuwa JK na serikali yake inahujumiwa na wakristo. pindi tamko likikamilika litawekwa hapa jamvini kwani ndio draft ya kwanza imekuwa tayari. ukumbi wa karimjee umelipiwa na mnene mmoja serikalini. leo mahubiri kwenye misikiti kadhaa DSM yamekuwa yakionyesha kuwa kila mara anapokuwa rais muislam basi anawekewa vikwazo na hata kudhalilishwa na wametoa mifano mingi ya Mwinyi na sasa JK.More 2 come later
Naomba waislamu msinielewe vibaya kwa maneno nitakayoandika hapa kwani ndivyo ninavyoamini mimi binafsi.
1. Binafsi naamini Waislamu kama watanzania wengine wana uchungu na uzalendo na nchi yao
2. Naamini waislamu kwa misingi na maamrisho ya dini yao, hawana nia ya kuvuruga amani wala kubagua watanzania wenzao kwa misingi ya dini
3. Naamini waisalmu wanapata haki kwa mgao sawa na wanavyopata wananchi wa dini zingine
Tatizo ninaloliona ndugu zangu ni kuwa kwa siku za karibuni (baada ya mchakato wa uchaguzi kuanza), waislamu wameanza kuchafuliwa kwa maksudi na watu wenye malengo ya kisiasa, kwa maslahi binafsi ya watu hao. Kwa bahati mbaya nahisi kuna udhaifu fulani katika system ya uislamu, inayosababisha wawe vulnerable na kurubuniwa kirahisi
1. Nahisi kuna ukosefu wa hirachy katika uongozi wa dini ya kiislamu. hapa namaanisha kuwa ni rahisi sana akajitokeza anayejiita shehe, Bakwata, au sijui nani akasema au kutenda kitu fulani kwa 'niaba' ya waislamu leo, na kesho akatokea mwangine, akawa kinyume nae, pia kwa niaba ya waislamu. Unaweza kuona mfano wa maandamano na mauji ya Arusha
2. Nina wasiwasi na nia ya BAADHI ya viongozi wa dini ya waislamu kuwa za kibinafsi zaidi
3. Nina wasiwasi na uaminifu wa BAADHI ya viongozi wa waislamu, kuwa na dalili ya kurubuniwa kirahisi na wanasiasa
4. Nina wasiwasi na elimu ya BAADHI ya viongozi wa waislamu, kwani pamoja na busara na uwezo wa asili juu ya masuala ya uongozi, lakini hatuwezi ku-underestimate umuhimu wa elimu katika uongozi
Kutokana na hayo, naona sasa kwa kuona kuwa wamezidiwa kila idara, CCM (au kikundi fulani ndani ya CCM), kimefanikiwa kuwarubuni baadhi ya viongozi wadhaifu wa waislamu, katika matukio tofauti, lakini katika mpango endelevu, na kuutumia uislamu kama ngao yao dhidi ya harakati za wanachi za kujikomboa kutoka katika udhalimu wa CCM
Nawaasa waislamu wote wenye nia njema kupinga na kulaani mpango huu wa kishetani wa CCM, wa kuwatumia kama ngao. Mtu yeyote ajue kuwa katika nchi ambayo hakuna dini yenye majority katika population representation, then hakuna chance kuwa move za udini na kidini zitakazowesha kundi lolote kupata maslahi yake, kinyume na matakwa ya walio wengi.
Waislamu wakumbuke kwamba, hata kama raisi atawapendelea katika nafasi za uteuzi, au mambo fulani madogo, hiyo naina maana ikilinganishwa na wanyanyaso wanayopata kama wananchi wengine katika nynja za kuichumi, afya, elimu n.k
Waislamu wakumbuke kuwa, kama wataamua kuisapoti serikali kwa kila kitu, eti kwa sababu raisi ni muislamu, ipo siku raisi huyom ataondoka madarakani, afafu wataona aibu kupinga mambo ambayo, ama leo wanayatetea, au yameanzishwa na raisi wa sasa.
Waislamu wakumbuke kuwa hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu anayempinga Kikwete kwa eti ni muislamu, bali anapingwa kwa kuwa ni dhaifu kiuongozi na kiutawala.
CCM wakumbuke kuwa wanapandikiza mbegu ambayo muda sio mrefu itawaangamiza hata wao
Hali kadhalika CCM wajue pia kuwa hata kama wana taarifa zozote zi 'kiintelijensia' kuwa pengine wapo wakristo wanaompinga JK kwa udini au wenye hila za maslahi ya kidini, njia muafaka ya kukabiliana nao sio kuzidi kupandikiza udini, bali ni kuukemea
Naamini wanaokuza udini ndani ya CCM ni wale wanaohitaji maslahi ya muda mfupi bila kujali mustakabali wa ama CCM au Tanzania katika siku zijazo.