kongamano la katiba UDSM Lahujumiwa

ZAma za propaganda zimepita, hizi ni zama za kutumia kichwa kufikiri. Nashangaa watu wanavitengo vya propaganda eti kuwashawishi waamini uongo kuwa ukweli. Uhuru, Habari leo, Tambwe Hiza na hata hao Waislam waandae Kongamano lao na mazimio yao yatakuwa yao. Lkn naamini kunawaislamu kibao wanauelewa na macho na masikio yao MKURUMA kesho.
 
Hilo kongamano la kidini halitawaokoa..sana sana litawazamisha zaidi.
Nyota mpya imeshaonekana
 
Kama waislamu hawatasimama na kuamua mambo yao wenyewe ipo siku watakuwa njia panda, maana tukiutafuta usafi a hao wanaowatumia kiukweli haupo, na hapa hata mafundisho ya uislamu wanakuwa wameyasaliti.
Huu udini tunaouona ukiletwa kwetu kwa njia hii ya ajabuajabu iko siku utatucost.
 

King Suleiman, ninakuunga mkono sana. Haya mambo ya wachovu wa kisiasa na watafuta maslahi binafsi yataleta balaa nchini mwetu. Wananchi tuangalie maisha yetu na mustakabali wa taifa letu na kizazi chetu cha baadaye.

Mtu anayetumia dini kwa ajili ya kujikinga na sauti ya umma juu ya uovu wake anaoufanya analeta balaa kabisa katika nchi hii. Tusikubali kudanganganywa na siasa za udanganyifu. Mungu epusha shida hii kwa watanzania.
 
huu ndio mchezo wa JK, ku divert attention ya kungamano la Katiba hapo UDSM, kama
vile Arusha eti wana CCM wanaomba kuandamana kumsifu meya wa Arusha, then kuweka
movie sawa polisi wamewanyima ruhusa hadi siku nyingine, all this ni kuchaganyanya na
kuwatoa ktk attention, ila watu wanajua, huu ni FIRST DEGREE YA UJINGA as they are nothing they have.
 
Jee kuifananisha CCM na Taliban ni udini au si udini?
 

Word!
 
Waislamu wanahaki ya kukutana na kama wanashutumu maaskofu wache wafanye hivyo na ni vema vyombo vya habari vikaandika mambo yote watakayoto!!!
Mwisho wa siku itajulikana kama ni ya kweli!!!
Kikwete alianza kusema hayo wakati wa uzinduzi wa bunge , akasema kuna udini , lakini mpaka sasa hana ushahidi wa mambo aliyosema !!!
Ametia aibu mbele ya jamii!!!
Kama kikwete kawatuma waislamu watamwaibisha !!!
Jambo ni moja ,tunataka viongozi wanaojari maaendeleo ya wananchi na siyo maendeleo ya rostam!!
Je, sabodo mustafa ni dini gani?? Mbona anachangia chadema???
Sabodo katoa mchango wa 10m kwa familia ya denis mkristo aliyeuawa arusha , lakini hajatoa kwa ismail ambaye ni muislamu mwenzake!!!
 

Heshima kwako mkuu. It's encouraging to have objective thinkers in our society.
 

Huo ni mkono wa JK, maana wote tunajua kuwa karata ya udini ndio mtaji wake maana ndg zetu hawa wanapenda sana kuegemea ktk masuala ya dini kama uwanja wao wa kujengea hamasa.
 
Waislamu wapendwa, ikumbukwe kuwa Kikwete huyo huyo mwaka 2005, alishinda kwa zaidi ya asilimia 80%. Wakati ule alipigiwa kura na watu wa dini zote. Leo anapo pigwa madongo, anapigwa na watu wa dini zote. Anapigwa madongo kwa sababu ya kuvurunda kwake, na si kwa sababu ya uislamu wake.

Anaporususu askari wake kupiga risasi, anawaamrisha wapige risasi (nyingi tu) kwenye kundi walipo watu wa dini zote. Risasi imemwua Mkristo na nyingine ikamwua Muislamu. Risasi nyingine zimejeruhi viungo vya watu wa dini zote na jinsia zote.

Mwaka 2005, alisema kuwa atahakikisha kuwa katika uongozi wake ataboresha miundo mbinu ya umeme ili nishati hii ipatikane kwa unafuu kwa wananchi walio wengi hususan wa vijijini. Leo, anaanza tu awamu ya pili, anakula matapishi yake mwenyewe kwa kubariki ongezeko la mgao wa umeme (ambao hata upatikanaji wake ni kwa kimtandao) la asilimia zaidi ya 18. Watu wakimshukia, utaambiwa kuwa, wanafanya hivyo kwa kuwa Rais ni Muislamu. Aaaaaaah jamani!!!

Udini haupo Tanzania, kilichopo ni kikundi cha watu wachache, waliopungukiwa sera kichwani, ambao wamejificha chini ya mwamvuli wa UDINI ambao pindi wananchi wakiwa kwenye mikakati ya kujadili mambo muhimu ya nchi yao; wao huibua masuala ya UDINI. Na kwa bahati mbaya, hutumia baadhi ya viongozi wa Kiislamu.

Tuwapotezee watu hawa, hawatufai hata kidogo. Wasituondoe katika mstari wetu wa kudai mabadiliko Aluta continua!!!
 

Wanaowatumia rafiki zangu waislam ni wale wasio WaTanzania halisi. Hawana uchungu na nchi. Majambazi wakubwa.....nk. Wanajua hata mkipigana, hola, wao wanasepa zao huko na kutuacha tunauana kipumbavu. Shame on them. Waislaam makini hawawezi kukubali kutumiwa. Pumbavu sana wanaowatumia wapendwa wangu aislaam. Mwizi ni mwizi, ni mwizi awe budha, mpagani, mkristu, mwislaam au hana dini. Hali kadhalika, mwadilifu anaweza toka dini yeyote ile, tena anaweza kuwa shekhe, padre, au hana dini kabisa......

WAKE UP BELOVED MOSELEMS, DO NOT BE USED BY HULIGANS.....
 
Wtz co wajinga kiasi hicho,wacha watoe matamko ya kijinga then yawabackfire
 
Naona mengi yameshasemwa na ni yale yale kwa humu' Uislamu ni udini". Naomba kuuliza yafuatayo:
1. Jee kongamano hili ili lipiku lile la Katiba limetangazwa kiasi gani kama lilivyokwishatangazwa hilo la mlimani?
2. Hivyo kwa hilo kongamano la Mlimani shughuli zote zitazuiliwa hata hawa Waislamu wasifanye shughuli yao?
Hivyo waislamu kama sehemu ya jamii hawana haki ya kufanya kongamaqno lao?
3. Hivyo kwenye uchaguzi uliopita watu wote walikuwa wapinzani wa Serikali ya Kikwete?
4. Hivyo katika hili kongamano la Waislamu maazimio watakayotowa yatakuwa maaazimio ya Waislamu wote na kongamano la mlimani litatowa msimamo wa kila mtu humu Tanzania? Ikiwa hivyo nahisi hatuna haja ya vyama kwani misimamo yetu si iko sawa?
5. Kwanini lazima Waislamu wapangiwe wakati fulani wafanye wanavyotaka?
6. Na kwanini Udini ni pale viongozi wa Kiislamu wanapotowa hoja zao wakati kila wakati viongozi wa Kikristo wanatowa matangazo kwa utashi wao? Wanawasiliana na wenzao wa Kiislamu kabla ya kutowamatamshi kama wadau kama tunavyotaka Waislamu wafanye?
Nafikiri hili la udini ni la Wakiristo kwani wao ndio wako sensitive na Waislamu wao huwa wanadai haki zao ambazo yeyote anaenyimwa ana haki ya kufanya hivyo. JF wacheni ukiristo (kwenu udini ni uislamu)
 
Hivyo unaweza ukaniambia eti nani ana uchungu wa nchi kati ya Wanasiasa wa pande zote mbili (CCM na upinzani)? Hebu nieleze panapo masilahi yao umesikia wakipingana? Mamilioni ya shilingi wanalipana na huku sisi tukilala hoi. Eti uchungu wa nchi yakguju Si chochote bali ni mapambano ya masilahi basi. Wakiristo na Waislamu wa kawaida ni watoto wa bandia tu!!
 
Ndiyo tatizo la wadogo zetu. Watakuwa wameambiwa kuwa kongamano litaambatana na kahawa, kashata, pilau, n.k maana hicho ndicho wanachokiabudu na kukitumikia siku zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…