KONGAMANO LA KATIBA UDSM: Richard Kasesera alitumwa na Kikwete,Lowasa na Rostam!

KONGAMANO LA KATIBA UDSM: Richard Kasesera alitumwa na Kikwete,Lowasa na Rostam!

Pasco_jr_ngumi

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2010
Posts
1,802
Reaction score
283
Wana JF.
Mlimsikia hoja za huyu 'kambwa mnuka Ufisadi'? Rafiki yangu wa karibu aliniambia alitumwa na mafisadi kuharibu hoja za wasomi. Mnasemaje?

Pia mi niliridhika sana na point za Lwaitama, Dogo aliyesema 80% ya nchi zenye katiba mpya dam ilimwagka, plus Shivji and Ulimwengu!
 
Kasesera ni mpumbavu tu wala hajatumwa!! Ila anajua kujipendekeza sana ili aonekane!! Namjua sana tangu akiwa kibo breweries na mashauzi yake, akajipendekekeza kwa Kikwete hata wana basketball wakamchagua kuwa mwenyekiti kwa kuogopa kuwa ametumwa na kikwete kugombea kumbe hakuna chochote, badala yake kikwete akajitoa kuwa patron wa Basketball na hakumsaidia kwa lolote katika uenyekiti wake!!! Kasesera hana kitu jamani wala tusimjadili hapa!!! tunaemjua hana lolote huyo
 
sidhani kama alitumwa, hulka zake tu............na maybe alikuwa nae anatoa mawazo yake............sio vema kushabikia umwagaji damu, vita sio kitu kizuri kama watu wanavyotajataja............Napata tabu kuelewa pale mtu anapohubiri ujumbe wa machafuko na watau wakashangilia. Istoshe kwenye hili swala la katiba lazima tujiandae kusikia mengi nya kufurahisaha na mengine ya kukera, la muhimu ni kuvumiliana.
 
Katiba mpya haiko chini ya Lowasa, Rostam wala Kikwete, sijajua mantiki ya kuwataja hawa watu.

Unazungumzia katiba ya watu milioni 40! kumbuka

1. Kuna wale ambao kweli kabisa hawajui katiba na hawaoni umuhimu wake, kama alivyosema Gad hapo juu, yaani hawako chapter moja na wewe! hawa watu wanahitaji kujibiwa kwa hoja
2. wako wanaoujua ukweli na wanafanya makusidi kulinda maslahi yao

kwa hali ya sasa kumtofautisha wa kwanza na wa pili ni ngumu, tukiwajua hawa wa pili unaweza hata kuwaua-rukhsa, ila utawajuaje?? is another big task

Tukiweza kujifunza kujenga hoja, tutawashinda, ukijifunza matusi hutaweza, maana unaweza ukakutana na maskini wa kutupwa still hataki katiba mpya na hana mpango nayo

sijui uliwaelewaje Shivji na Ulimwengu, ni waongeaji wazuri ila ukichukua idea zao practically unaweza ukaipata katiba baada ya miaka 2000! please use your head as well no matter who said.! tunawajua vizuri sana hawa watu wawili na tunajua upande gani waliopo!!!!! ni ngumu kuambiwa na kukubali sasa, let me reserve for now

In short we need new katiba na majina ya akina Lowasa, Rostam kamwe yasiingizwe they are nothing, issue za ufisadi hata wewe ni kipeleleza sana unaweza ukawa ni fisadi mzuri tu, nchi hii wengi wanajifanya clean ukifuatilia ni afadhali akina Lowasa na Rostam, na kama kweli hao jamaa wanapinga katiba mpya kwa sababu ya ufisadi wao, basi BELIEVE ME they are no only ones!
 
Hoja ya haja ya kutaka Katiba mpya isichanganywe na ufisadi, udini wala ukereketwa!
 
ingawa simjui vema kasesera lakini hakuna alilolifanya kwenye basketball family. hakuiendeleza. uchaguzi wake ulitawaliwa na rushwa ndio akamshinda msofe. ni opportunist kama walivyo wanasiasa wengi wanapoanza. ukizingatia na vijisenti vimemtembelea basi balaa.
 
Mh!!! Najaribu kufikiri uwepo wa kasesera pale kwenye kongamano, naamini hakutumwa na mtu yeyote ila ni victim of his own fate. Ofcourse ana haki ya kuchangia ila sidhani kama alikuwa na nia thabiti ya kuchangia mada. Alizungumza ili awe recognized (kwa lugha nyepesi kutafuta umaarufu) na sio kwa mantiki ya kuchangia mjadala ule wa katiba. Tatizo hakujipanga.
 
Mh!!! Najaribu kufikiri uwepo wa kasesera pale kwenye kongamano, naamini hakutumwa na mtu yeyote ila ni victim of his own fate. Ofcourse ana haki ya kuchangia ila sidhani kama alikuwa na nia thabiti ya kuchangia mada. Alizungumza ili awe recognized (kwa lugha nyepesi kutafuta umaarufu) na sio kwa mantiki ya kuchangia mjadala ule wa katiba. Tatizo hakujipanga.

Umenisemea mawazo yangu..thanks
 
lakini haishangazi, siyo mara ya kwanza kumwona kwenye mijadala ya wazi na kila alipopewa mic aliharibu! Nafikiri ndiyo kwanza anajifunza kuwasilisha hoja ambazo nafikiri hana!
 
Back
Top Bottom