Kongamano la Kodi Kitaifa, Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Januari 11, 2023

Kongamano la Kodi Kitaifa, Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Januari 11, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Lenye lengo la kupokea maoni kuhusu maboresho mbalimbali ya tozo na ada kuelekea uandaaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24




Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema maendeleo yoyote Nchini lazima yawe na uhusiano wa moja kwa moja na kodi

Amesema “Kwa Nchi zenye hali mbaya, zile za mwisho kwenye umasikini ambazo hazina vyanzo vya kodi vyenyewe ndio wanaweza kutegemea vyanzo vingine kama misaada, lakini Nchi ambazo zimeshaendelea kama ya kwetu hata ukikopeshwa malipo yake yatatokana na kodi.

“Ili uonekane unakopesheka, unapimwa kama unaweza kukusanya kodi, kipimo kikubwa ni kuona makusanyo yako kama yanaweza kurejesha deni.”

Aidha, amewataka watendaji wa Serikali kubadilisha mtazamo wa ukusanyaji wa kodi kwa kuwaheshimu watu wanaowekeza kiuzalishaji ili walipe kodi.

Ameyasema hayo leo Januari 11, 2023 jijini Dar es Salaam katika kongamano la kodi kitaifa.


Mwigulu: Vijana milioni 1 wanaingia kwenye soko la ajira kila mwaka
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema soko la ajira linatakiwa kuboreshwa katika sekta binafsi kwa kuwa kuna vijana wengi wanaoingia kwenye la ajira kutoka shuleni na vyuoni ambapo Serikali haina uwezo wa kuajiri wote.

Amesema “Kuna wanaohitimu darasa la 7 na hawaendelei sekondari, wapo wanaohitimu kidato cha nne, cha 6 na hawaendeleo, pia wapo wahitimu wa vyuo vya kati na vyuo vikuu, jumla kwa mwaka ni milioni 1 na wanaingia kwenye soko kutafuta ajira.”

Ameeleza kwa idadi ya taasisi za Serikali, Wizara, Halmashauri idadi hiyo haitoshi na wanahitaji sekta binafsi iliyo imara kuweza kuhakikisha watu wote hao wanakuwa kazini.
 
Lenye lengo la kupokea maoni kuhusu maboresho mbalimbali ya tozo na ada kuelekea uandaaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24....
jamaa kakubali kwenye kabango kake kwamba Maendeleo ya watu na si maendeleo ya vitu (madaraja, reli, mabwawa ya maji nk.

Development MUST be people centered.
 
Wanao lalamika kelele za kodi na mamlaka za kodi ndio wakati wenu/wetu huu

Vyama vya siasa (wakina sugu) wasanii (wakina Nasib) na wananchi wengine, huu wakati muutumie/tuutumie vyema, tusije kuwa na majuto huko mbele

Lilipita kongamano la wadau wa usafirishaji...

Limepita kongamano la waziri wa ardhi juzi

Yote ni kwa manufaa ya wananchi, tuyatumie vyema haya majukwaa
 
jamaa kakubali kwenye kabango kake kwamba ni Maendeleo ya watu na si maendeleo ya vitu (madaraja, reli, mabwawa ya maji nk.

Development MUST be people centered.
Wewe unaona hayo wanayofanya ni maendeleo ya watu au ya vitu?
Maana unaweza kuambiwa ni ya watu kumbe ni ya watuvitu
 
Ruzuku ya Chadema ni kodi za wananchi
CDM haijawahi kuchukua ruzuku, CCM ndiyo inakomba Ruzuku yoote 1.33billion kwa mwezi - hii ni baada ya kupora uchaguzi mkuu 100% chini na mwendasafari.

Kwa hiyo watafute uwahoji hizi pesa zote wanazifanyia nini wakati biashara ya kuunga juhudi haipo siku hizo.
 
Back
Top Bottom