Wengi wetu neno dijitali tulianza kulifahamu wakati ule mfumo wa televisheni zetu unahama kutoka analogia kwenda dijitali, neno hili lilipata umaarufu sana lakini ukiuliza maana halisi ya dijitali na msaada wake wengi wetu tulikuwa hatufahamu.
Katika harakati zangu za kulijenga taifa letu leo nilipita maeneo ya Kijitonyama pale nilikuwa na mdau wangu mmoja tunayefanya naye biashara, ilitubidi kuingia pale Millenium Towers katika tawi la CRDB kufanya muamala, tulipoingia ndani mhudumu aliyekuwepo kwenye floor alituuliza huduma tunayohitaji na kisha kutuelekeza katika dawati la "Fahari Fasta" nafahamu wengi hatuijui hii, lakini leo ndio hasa nilijua maana ya dijitali na umuhimu wake katika kurahisha upatikanaji wa huduma, mwanzoni nilidhani ni ngumu lakini baada ya kupata maelekezo, nilijihudumia mwenyewe kirahisi kabisa.
Kwa mara nyengine tena nilijikuta nikijivunia kuwa mteja wa benki hii ya kizalendo ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikiongoza katika kubuni huduma nyingi za kidijitali kama SimBanking, Internet banking, FahariHuduma Wakala pamoja na huduma ya akaunti ya vikundi kupitia SimAccount, vyote vikituwezesha sisi wateja kupata huduma bila kutembelea tawini.
Niseme tena Kongole Benki ya CRDB, Watanzania tunajivunia 🙏