Kongole Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule

Ichwampaka

Senior Member
Joined
Nov 19, 2018
Posts
145
Reaction score
118
Nampongeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule kwa utumishi wake uliotukuka. Tumpe mtu maua yake anapostahili sawa na tunavyowakosoa.

Sifa kuu za DC Mtambule ni hizi:
1. Msikivu sana, katika kupokea mashauri, kero na malalamiko ya wanachi na watendaji

2. Ni mfuatiliaji mzuri wa mambo yanayohusu wananchi na utendaji

3. Hana papara wala jazba anapotoa maagizo lakini usipotekeleza utamwelewa vyema

4. Hana urasimu na umangimeza kumuona; ili mradi yupo ofisini atakusikiliza

5. Wakati wote yeye anatafuta ufumbuzi wa tatizo kuliko kuhangaika na stori na victimization

6. Ni mshirikishaji mzuri sana, hakuna jambo anafanya bila kuhusisha wahusika kama ni watendaji au wadau

7. Hapendi kuahidi au kusema uongo lakini pia hapendi kudanganywa

8. Always anakupa second chance, hakuadhibu on the first instance au kama kuna jambo hujafanya vizuri atakupa ukomo wa kulitimiza, ukishindwa ndio rungu lake linatua.

9. Ni mshuhudiaji wa mambo sio mtu wa kuepekelewa taarifa tu na kukaa ofisini

10. Anahimiza sana maendeleo, kujali afya, maadili, usafi wa mazingira, kulipa kodi, utatuzi wa migogoro ya kidini, kijamii na mambo ya ardhi.

Haya ndio nimeyaona kwake. Anaweza kuwa na mapungufu kama tulivyo binadamu wote ila huyu DC ukimuweka kwenye mizani uzuri wake unashinda mapungufu yake kwa zaidi ya 95%.

Hongera sana Rais wetu Dr. Samiah Suluhu Hassan kutupatia kiongozi bora kabisa.
 
Utakuwa papasi wake kama si kiroboto.
 
mie nampongeza RC wa chuga
 
Kuna mgogoro mkubwa sana wa taasisi ya dini moja ambao umedumu miaka 12 ameweza kuutatua bila hata kujitangaza au kupiga picha na viongozi wa pande zote mbili kuashiria kumalizika kwa mgogoro kama ambavyo wengine wangefanya.
 
Kushirikiana na viongozi mbalimbali ameweza kulipatia ufumbuzi tatizo la madada poa waliokuwa kero kubwa sana mitaa ya nyuma ya ''Ambience Club''.
 
Hapana hanituma; hata jina hanifahamu ila kwa sura nina uhakika ananifahamu nikimkumbusha mawili matatu atanikumbuka.
 
Back
Top Bottom