KONGOLE STARS, ILA TULIWAVURUGA SANA VIJANA
KIuhalisia Tanzania imeyaaga mashindano ya AFCON rasmi na hata ndugu zetu Kenya nao wameyaaga tu licha ya kutujeruhi maana watapigwa tu mechi na Senegal.
Hata hivyo pamoja na maumivu tuliyonayo tuukubali ukweli huu:
*1.VIJANA WAMETIMIZA WAJIBU WAO*
Wachezaji wetu tuwape kongole. Wamepambana kuweka historia ya kufuzu Afcon na sote tulifurahi sana lakini tukiri hawakupata wasaa wa kujiandaa kwa fainali za Misri.
Hata kambi ya Timu haikuwepo. Walipoungana tu Dar ghafla wakatangulia Misri...Hatukuwasaidia vijana kupata utulivu kwenye kambi ya maana.
*2.SERIKALI IMETIMIZA WAJIBU WAKE*
Ukiitazama hii timu imelelewa sana na Serikali hasa kuingia moja kwa moja kwa Mhe. Rais mwenyewe kusaidia timu kwa fedha mara kadhaa, kuwaita Ikulu kuwapa moyo na hata Waziri wa Michezo mara kadhaa amekuwa akiongoza Harambee kuichangia timu.
*3.MASHABIKI SIO PIERRE WALA WABUNGE WALA MAKONDA*
Nao walitimiza la upande wao hasa wakati wa kufuzu ingawa wengi wa hamasa hawakupatiwa fursa kwenda Misri kuweka hamasa zaidi.
*YA KUTAFAKARI ZAIDI*
1. HIVI TFF WAPO?
Najiuliza kuhusu hawa jamaa, sikuwaona Kkabisa wakihamasisha team vya kutosha, wakijenga nguvu ya hamasa ya michezo na mara nyjngi ilibidi hadi kuisikia Serikali ndio ujue Stars ipo.
Najiuliza hawa jamaa wapo wapi na walikuwa wanafanya nini kuisaidia team?
*2.AMUNIKE NAYE YUPO TU*
Huyu baba jamani wanaemjua wanafahamu kuwa si kocha, msanii tu, hana hamasa hana ufundi.
Tunaweza kusema tumepambana na Senegal wakali...sasa hata dhidi ya Kenya???
Timu inapoteza concentration kila muda unavyozidi kwenda. Nilishangaa ghafla akiwa Misri akateua benchi jipya hasa la makocha wa viungo...hivi alikuwa anataka kufikia kitu gani...mpaka sasa najiuliza TFF waliruhusu hii na kwa nini?
*PIERRE LIQUID, MAKONDA NA WABUNGE WETU*
Kuna wakati tunafanya mambo ktk masuala ya kitaalamu mpaka unashangaa, unaumia tu.
Hivi katika mashabiki wa kuwapa hamasa vijana uwanjani Pierre Liquid ndio tumeona wa maana?
Mlevi anayelewa hadi kujilalia hoi, uwanjani kwenyewe alikwenda mechi ya mwisho tu tena wala hata uwanjani hakuingia zaid ya kuishia baa za nje pale Taifa na kupiga gambe ndie tulitarajia akasimame jukwaani kutoa hamasa?
Wako wapi wahamasishaji wa muda wote wa klabu mbalimbali za ligi kuu?
Hatukuweza kuunda kikundi kimoja wakapelekwa Misri kuwapa hamasa wachezaji wetu na kumpa stress adui?
WABUNGE; Bado najiuliza mpaka leo, hawa nao walikwenda Misri kufanya nini?
Walikwenda kutengeneza nongwa, fitna, majungu na waliiharibu saikolojia ya timu katika mechi ya kwanza tu. Wallahi hawa dah!
*PAUL MAKONDA*: Mpaka sasa sijaelewa yaani huyu na manongwa yake, mikosi, laana, mabalaa, kujifaragua, kuigawa jamii, ujinga na kauli tata na za dharau muda wote ndio tulimpa kuwa "mmliki" wa Timu ya Taifa?
Sielewi; kuna mda alikuwa anaongea kama Waziri wa Michezo, kuna mda kama yeye ndio TFF, kuna mda kama yeye ndio kocha, kuna mda kama yeye ndio captain wa team au mmiliki wa timu.
Nilicheka sana...kuna mda wachezaji walikuwa wanahitaji kupumzika, kufocus ktk game na kuficha mbinu zao na saikolojia zao adui asijue, jamaa lilipotua tu Misri likaanza ujinga wake; mavikao, mapress conference yasiyo ya kimkakati, kutoa maagizo kama kocha, kuongoza dua kama sheikh au askofu, kuratibu mipango hewa ya team n.k.
Yani kwa kifupi tu tuliiharibu mno kambi ya team ikakosa utulivu, mshikamano, ari, hamasa na nguvu ya kimapambano.
Nasikia Makonda alivyotua tu Misri mpasuko mkubwa ukatokea tena kambi ya Stars, akawa kila kitu...kuanzia kocha, kocha wa viungo, saikolojia, logistics za team, nani acheze, mipango ya posho na kila kitu akawa yeye, team ikazidi kukosa usimamizi na uendeshaji wa kitaalamu.
Tumewaachia wapi wajenga saikolojia kama akina Peter Tino na wale nyota wenzake wa zamani?
Serikali imetimiza wajibu wake, wachezaji pia na sisi madhabiki tuliobaki bila kwenda Misri na kukodoa macho[emoji15][emoji15][emoji15] na kuongoza sala za kimya kimya popote tulipo nchini pia tumetimiza yetu.
Lakini wapo watu tuliowatuma kuwa karibu na team wameifanya iwe mbali na utimamu!
Ahsanteni
Sheikh Kipozeo wa Soka, Mkuranga, Pwani.