Pre GE2025 Kongwa, Dodoma: TASAF yakabidhi nyumba za walimushule ya sekondari Chitego

Pre GE2025 Kongwa, Dodoma: TASAF yakabidhi nyumba za walimushule ya sekondari Chitego

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameshukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbal inayotekelezwa na TASAF nchini.

Salimu Mshana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba za walimu (familia nne) wa shule ya Sekondari Chitego katika kijiji cha Chitega Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma

Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Mshana amesema TASAF ipo nchi nzima na jitihada mbalimbal zinafanyika kwa uongozi na kama inavyojulikana rasilimali ni kidogo lakini kwa kadri inavyogawanywa viongozi wanapambana kufanikisha ufumbuzi wa matatizo kwa wenye uhitaji Nchini.

"Ukiona jambo limefanyika kuna watu nyuma yake na sisi kama TASAF tumeweka fedha lakini bado haziwezi kufanya kazi zinazofanyika bila mkono wa Seeikali na kushirikisha wananchi.

Aidha Mshana amesema dhana nzima ya TASAF ni ushirikishwaji wa jamii na ni msingi mkubwa katika utelelezaji wa miradi hiyo ya TASAF.

Hata hivyo Mshana ametoa rai kwa wanufaika wa nyumba hizo kuhakikisha wanazitunza

" Kwa upande wa TASAF tumemaliza ila nasisitiza ni vyema ila baada walau hata miaka mitatu ukarabati katika nyumba hizi ufanyike, na walimu wetu sasa angalau hizo familia nne zimepata mahala pazuri pa kukaa na tuna imani wataweza kuongeza ufauli kwa wanafunzi kwa kuwa wanaishi jirani na shule hii "

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Chitego Born Mwakalasya mmoja wa wanufaika wa nyumba hizo amesema wanaishukuru Serikali kupitia TASAF kuwaondolea changamoto kwa kuwa walikuwa wanaishi mbali na shule, hivyo kuwafanya kuwa karibu na maeneo ya shule na swala zima la utoaji wa huduma kwa wanafunzi litaongezeka kwa kuwa mda mwingi watakuwa katika mazingira ya shuleni hapo.
Screenshot 2025-03-02 162016.png
 
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) unapatiwa fedha kutoka serikalini!
Inachukua fedha hizo hizo kwenda kujenga miradi ya serikali!
Swali: Kwanini serikali isipeleke fedha hizo Moja Kwa Moja,kwenye miradi yake??.
KAZI na madhumuni ya TASAF ni haya???
 
TASAF ni ya watu masikini. Walimu ni matajiri?
 
Back
Top Bottom