Doctors, naomba msaada. Nina miezi kama minne nimekuwa nikisumbuliwa koo linalowasha kama mtu anayekaribia kupata mafua au kikoozi. mwanzoni hizi zilikuwa dalili za mafua au kikoozi kwangua. Tatizo la sasa nimetumia antibiotics nyingi lakini sipati nafuu, zinatuliza tu ana baada ya siku mbili hali inajirudia, na siku nyingine napiga chafya mpaka macho na masikio yaniniuma. Nifanyeke niweze kuondoa tatizo? very urgent please.
Jaribu kucheck UTI
nashukuru sana mkuu, inawezekana ikawa allergy, nitajaribu kufanya allergy test,uti ni maambukizi ya njia ya mkojo (urinary tract infection)...sa inahusiana vipi na koo?! Maelezo yako yanarandana kabisa na 'allergy'. Kuna kitu kwenye hewa (perfume, mafuta, sabuni, vumbi, pollen, etc) ambacho una allergy nacho, unapokivuta kwenye hewa basi airway inareact na kukusababishia huo muwasho, chafya, mafua etc.
Antibiotics haziwezi kukusaidi katika tatizo lako, kwa sababu huna bacterial infection...labda unaweza pata bacterial infection days baada ya hiyo reaction. Sikushauri uendelee kutumia antibitics.
Nenda hospitali kafanye 'allergy test', itakupa idea vitu gani unareact navyo..kisha uviepuke. Na unapopata reaction unahitaji dawa za jamii ya 'anti-histamine' ambazo zenyewe husimamisha hiyo reaction. Nenda kwa daktari kwa ajili ya alergy test na ushauri zaidi.