Korea kama hauna degree haupewi mke, Ifike mahala kama hauna degree usigombee ubunge

Nchi sasa imekuwa na wasomi wengi lazima tukubali ,hivyo lazima tubadilishw hata baadhi ya vipengere wakati mbunge Msukuma anaomba mfumo wa elimu ubadilishwe pia na sisi tunaomba kipengere cha sifa ya mtu kugombea ubunge kibadilishwe hiwe lazima hawe degree order.

Kwa uandishi huu na kiwango hiki cha degree bora hata huo ubunge wapewe STD IV B.
 
Wengi mnaopinga ni Standard VII B kama wewe
 
Ndio maana nimesema dunia haipo tena kwenye 3K's hata hapa bongo kuna ubaguzi kama unaenda kuoa binti mwenye degree expect mahali kuwa kubwa inaanzia M wakati mahali za form 4 ni 400K fanya uchunguzi.

Kwa Korea ni ngumu kwenda kuoa binti kama hauna degree ni aibu kwa familia ,watu wasio na degree unawatafuta kwa torch sawa na kutafuta bikira Buza.
 
Yani una pesa alafu uone si kitu kisa huna degree?

Hauko serious mkuu
Kuwa na pesa bila degree ni sawa tu na kuwa na mke mzuri halafu hauna mtoto.
Tafuta wazee wenye pesa wasio na shule kaa nao uwadadisiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Degree unaipima kwa uandishi wa insha kweli wewe umeishiwa au unadhani wote tulikaa darasani kuchukua degree za kiswahilo na lugha kama wewe???πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kuwa na pesa bila degree ni sawa tu na kuwa na mke mzuri halafu hauna mtoto.
Tafuta wazee wenye pesa wasio na shule kaa nao uwadadisi[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Unakula hiyo degree?

Digreeinatakiwa uigeuze iwe hela ndio uone faida yake! Lakini kama huna hela na una degree utaonekana ni taka tu.

Lakini mwenye hela ila hana degree hata kwenye vikao mawazo yako ya kidegree yanatupwa kapuni ila ya mwenye hela ndio yatafanyiwa kazi.
 
Hii nchi ni yetu sote. Wengi waliyoikomboa hata shule hawakwenda. Leo hii kuna umuhimu gani wa kubagua uwakilishi wa wananchi kwa kuangalia elimu.

Ukifika kwenye kutunga sheria wabunge darasa la saba warudi kwa wananchi wanaowawakilisha wachukue maoni yao sio kama walivyo wasomi kama Talimba kuongea bungeni ambayo hawajatumwa na wananchi.
 
Naona unaleta debate ya pesa bora kuliko elimu.Endelea na debate yako lakini nakuhakikishia haitopita awamu mbili hicho kipengere cha darasa la saba kuwa mbunge kitabadilisha ,mods wataweka kumbukumbu ya nyuzi kama hii hapa tuombe uzima tu.
 
Naona unaleta debate ya pesa bora kuliko elimu.Endelea na debate yako lakini nakuhakikishia haitopita awamu mbili hicho kipengere cha darasa la saba kuwa mbunge kitabadilisha ,mods wataweka kumbukumbu ya nyuzi kama hii hapa tuombe uzima tu.
Ni sawa kabisa!

Lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba degree yako haitakusaidi kama hutaigeuza iwe hela labda uitumie kupata huo ubunge kama hivyo.
 
Kwahyo walio disco mke wataskia kwa jirani
 
Kwahyo walio disco mke wataskia kwa jirani
Upate bahati mwanake akupende kweli kweli baada ya wazazi kujiridhisha unapewa interview na baba mkwe ukishinda unaweza lipa posa ukamuoa.Lakini baada ya kupita interview lazima tena upeleke majibu ya vipimo vya afya na bank statement.

Je utachomoka hapo??wataangalia mpaka unamiliki nyumba ya aina gani ,model ya gari ,historia ya familia yako n.kπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kishimba hana degree lakini ana point kuliko madegeree sababu ana exposure
 
............. Kama wa darasa la saba anaweza kuwasemea vizuri changamoto zao huko mjengoni ni hakika atapata kibali kwao. Kwa maana nyingine wananchi ndo wanaamua kwamba tumpe huyu mwenye degree au wa la saba..........

Katiba ndivyo inavyotaka. Lakini 2020 haikua hivyo, chama cha kijani tangu kwenye kura za maoni, kiliamua nani awe mbunge, maamuzi hayakua ya wananchi. Tena to be precisely, Mwenyekiti wao ndiye alikua final.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…