Korea Kusini yaondolewa vizuizi vya makombora. Ruksa sasa kuunda makombora yenye uwezo mkubwa zaidi!

Korea Kusini yaondolewa vizuizi vya makombora. Ruksa sasa kuunda makombora yenye uwezo mkubwa zaidi!

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
5,500
Reaction score
8,060
Habari!

Marekani imeiondolea Korea Kusini vizuizi ama ukipenda waweza kuita vikwazo vya muda mrefu (miaka 42) juu ya uwezo wake wa kutengeneza makombora. Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in alitangaza uamuzi huo Ijumaa kufuatia mkutano wake na Rais wa Marekani Joe Biden hivi karibuni jijini Washington.

Vizuizi vya Marekani hapo awali viliweka ukomo kwa Korea Kusini kuendeleza au kuwa na makombora yenye masafa zaidi ya kilometa 800 sawa na maili takribani 497.

Mnamo mwaka 1979, Korea Kusini iliingia katika makubaliano ya kuweka kikomo cha makombora cha kilometa 180 sawa na maili 112 kama sharti maalumu ili iweze kupatiwa teknolojia ya utengenezaji makombora kutoka Marekani.

Kutokana na kuongezeka kwa vitisho vya kiusalama kutoka Korea Kaskazini, miongozo ya makubaliano hayo imerekebishwa mara nne mpaka sasa. Marekebisho ya 1997 yaliiruhusu Korea Kusini kutengeneza kombora la balistiki lililokuwa na uwezo wa kubeba silaha (warhead) ya kilo 500, lenye uwezo wa kusafiri kwa umbali wa hadi kilometa 300.

Marekebisho mengine yalifanywa mnamo mwaka 2012 ambayo yaliongeza uwezo wa makombora ya balistiki hadi kilometa 800 (sawa na maili 497) na uzito wa silaha wa kilo 500.

Kufuatia jaribio la sita la nyuklia la Pyongyang (Korea Kaskazini) mnamo mwaka 2017, Korea Kusini na Marekani zilikubaliana kuondoa kikomo cha uzito wa silaha, na marekebisho mengine yalifanywa mnamo 2020 ili kuruhusu utengenezaji wa roketi za anga za mbali (solid-propellant space rockets).

Vikwazo ama vizuizi vyote sasa vimeondolewa rasmi baada ya miaka 42. Hii ina maana kuwa, Korea Kusini sasa inaweza kutengeneza makombora ya balistiki yasiyo na kikomo cha uzito wa silaha na yenye uwezo wa kuzifikia shabaha za mbali zaidi ya Rasi ya Korea.

Matarajio ya wengi (nikiwemo mimi) ni kuamshwa kwa mashindano makubwa ya silaha hususani makombora ya balistiki katika Rasi ya Korea. Uwezo wa kiuchumi na kiteknolojia wa nchi ya Korea Kusini hivi sasa unatosha kwa kiasi kikubwa kuiwezesha nchi hiyo kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya makombora.

Pia, hii inatazamwa na baadhi ya wachambuzi kama njia mojawapo ama hatua ya Marekani kama sehemu ya mkakati wa kukabiliana na mataifa kama China katika eneo hilo kupitia mshirika wake, Korea Kusini.

Waweza kuisoma taarifa hii [kwa ukamilifu wake] kupitia vyanzo vifuatavyo:
1. Defense News | US lifts missile restrictions on South Korea, ending range and warhead limits
2. The Korea Times | Seoul's 'missile sovereignty' comes as double-edged sword
3. The Defense Post | US, South Korea scrap bilateral missile guidelines
 
Kombora la balistiki la Hyunmoo la Korea Kusini. Hili ni moja ya makombora yaliyoundwa chini ya vizuizi vilivyokuwepo hapo awali.

1622290712426.png

1622289741649.png
 
Hapa ni kumfunga speed governor Kiduku, ule upande wa pili Mjapan naye anataka kuimarisha jeshi vizuri kabla ya pembe za m China hazijawa ngumu kukata.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Mjapani ana teknolojia kubwa sana ya uundaji wa roketi za anga za mbali. Ukiachana na hilo, pia ana asilimia zipatazo 90 za madini yote yanayotumika kuunda silaha za nyuklia (weapon-grade plutonium) kwa nchi zisizo na silaha hizo duniani.

Hizi asilimia 90 za weapon-grade plutonium ni ulinzi tosha kabisa (deterrence) kwa nchi isiyo na silaha za nyuklia kwa sababu zinaweza kutumika kuunda idadi kubwa ya silaha kwa muda mfupi sana (miezi 6 hadi 12). Ndio maana wataalamu wa masuala ya nyuklia wanapenda kuutumia msemo mmoja maarufu sana kwamba: "Japan has nuclear bomb in the basement".

Kitu kimoja ambacho kinaizuia zaidi Japan kuunda silaha hizo ni upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi (public opposition) dhidi ya silaha hizo ukizingatia kuwa Japan ni nchi ambayo imekwisha pata uzoefu wa madhara ya silaha za nyuklia. La sivyo, hivi sasa ingekuwa ni nchi ya tatu kwa wingi wa silaha za nyuklia baada ya Marekani na Urusi.
 
Mjapani ana teknolojia kubwa sana ya uundaji wa roketi za anga za mbali. Ukiachana na hilo, pia ana asilimia zipatazo 90 za madini yote yanayotumika kuunda silaha za nyuklia (weapon-grade plutonium) kwa nchi zisizo na silaha hizo duniani...
Kupitia komenti hii leo ndo nimejua ni kwanini US aliwai fasta kumsainisha dili la amani na kumlimda mjapan baada ya matukio ya iroshima na Nagasaki. Nje na hivyo uenda leo tungelikuwa na history pacha juu ya matukio ya atomic. Kumbe, mjapan ana kitu adhimu kiasi hiki!!.

Na yote katika yote,Japan ndo Giant ya huo ukanda.. N/K hata leo hawana uwezo wa kwenda vitani na Japan japo kwasasa hawajishughulishi na masuala ya kijeshi kivile.
 
Dunia inazidi kujilimbikizia silaha za kila aina kwa malengo ya kufanya maangamizi...
na yote haya mlengwa mkuu wa kuangamizwa ni mwanadamu huyo huyooo
kazi ipoooo
 
Dunia inazidi kujilimbikizia silaha za kila aina kwa malengo ya kufanya maangamizi...
na yote haya mlengwa mkuu wa kuangamizwa ni mwanadamu huyo huyooo
kazi ipoooo

Maskini wanapowezeshwa hupenda kuonyesha pembe. Hili ndilo lililotokea baada ya China kuwezeshwa.Mkakati wa marekani unaweza kuwa ni hatari sana kwa usalama wa China na Asia yote.
 
Mjapani ana teknolojia kubwa sana ya uundaji wa roketi za anga za mbali. Ukiachana na hilo, pia ana asilimia zipatazo 90 za madini yote yanayotumika kuunda silaha za nyuklia (weapon-grade plutonium) kwa nchi zisizo na silaha hizo duniani.

Hizi asilimia 90 za weapon-grade plutonium ni ulinzi tosha kabisa (deterrence) kwa nchi isiyo na silaha za nyuklia kwa sababu zinaweza kutumika kuunda idadi kubwa ya silaha kwa muda mfupi sana (miezi 6 hadi 12). Ndio maana wataalamu wa masuala ya nyuklia wanapenda kuutumia msemo mmoja maarufu sana kwamba: "Japan has nuclear bomb in the basement".

Kitu kimoja ambacho kinaizuia zaidi Japan kuunda silaha hizo ni upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi (public opposition) dhidi ya silaha hizo ukizingatia kuwa Japan ni nchi ambayo imekwisha pata uzoefu wa madhara ya silaha za nyuklia. La sivyo, hivi sasa ingekuwa ni nchi ya tatu kwa wingi wa silaha za nyuklia baada ya Marekani na Urusi.
Hawa jamaa hawa wajaps nawaheshimu sana, Jamaa wana miakili balaa,wachapa kazi mno halafu ni makauzu hatari yani hawanaga masihara kabisa kwenye kazi zao [emoji119][emoji119]
 
Maskini wanapowezeshwa hupenda kuonyesha pembe. Hili ndilo lililotokea baada ya China kuwezeshwa.Mkakati wa marekani unaweza kuwa ni hatari sana kwa usalama wa China na Asia yote.
Ni hatari hata kwa marekani mwenyewe kwa baadae, hakuna rafiki wa kudumu...si Unaona China anavyomvimbia sasa hivi US, kashasau kuwa kufika hiyo levo ni jitihada za US.
 
Ili taifa lako liwe na amani na furaha na maelewano kwa mataifa mengine, kaa mbali na marekani na wala msishirikiane kwa chochote.
 
Back
Top Bottom