Korea Kusini yaonesha nia ya kutaka kuwekeza kwenye Sekta ya maji Dar na Pwani

DAWASA

Official Account
Joined
Oct 7, 2010
Posts
201
Reaction score
121
Ujumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini imetembelea miradi ya maji ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kujionea jinsi gani Serikali ya Korea inavyoweza kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kutoa huduma ya majisafi kwa wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.

Akizungumzia ziara hiyo, Msimamizi Kitengo cha Usimamizi wa Upotevu wa Maji DAWASA, Mhandisi Tyson Mkindi amesema ujumbe huo umekuja DAWASA kwa lengo la ushirikiano wa kuendeleza miradi mbalimbali ya maji sambamba na kuangalia namna ya kusaidia kuzuia upotevu wa maji.



​
"DAWASA tumepata bahati ya kutembelewa na ujumbe kutoka Serikali ya Korea Kusini, ambao umefika kwa nia ya kuangalia fursa za kuwekeza katika miradi, mitambo ya maji pamoja kutupatia mbinu mbadala za kuzuia upotevu wa maji," amesema Mhandisi Mkindi.

"Ujumbe huu umeanza kwa umetembelea Mtambo wa Uzalishaji Maji Ruvu Chini pamoja na mataki ya kuhifadhi maji kwa lengo la kujifunza na kupata mwanga wa namna ambavyo Serikali ya Korea Kusini inaweza kushirikiana na Mamlaka kufanya uwekezaji wa kupanua mitambo yetu ya maji itakayosaidia kuongeza utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi," ameongeza Mhandisi Mkindi.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkuu kutoka Serikali ya Korea Kusini, Mkurugenzi wa Ulsan International Development Cooperation Center (UIDCC), Chanmin Park amesema Serikali yao imeendelea kuwa na utayari wa kushirikiana na DAWASA kuboresha huduma za maji kwa kuangalia sehemu muhimu za kuboresha huduma hususani katika upanuzi wa mitambo ya uzalishaji maji na uzuiaji wa maji yanayopotea baada ya kuzalishwa.
​
"Tumefurahi kupita Mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini tumeona jinsi gani DAWASA inazalisha maji kwa kiasi gani na mahitaji yalivyo kwa wananchi kuwa ni mengi" amesema ndugu Park.
​
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2026-04-22 at 10.02.51.jpeg
    98.9 KB · Views: 13
  • WhatsApp Image 2026-04-22 at 10.05.28.jpeg
    112.4 KB · Views: 15
  • WhatsApp Image 2026-04-22 at 10.03.20.jpeg
    109.1 KB · Views: 13
  • WhatsApp Image 2026-04-22 at 10.05.28.jpeg
    112.4 KB · Views: 14
Kwani tatizo letu kuu ni uzalishaji mdogo wa maji mtamboni, au ni uchakavu wa mabomba yanayoshindwa kufikisha maji yaliyopo kwa mwananchi?
 
Hata hili la maji yetu tunataka wawekezaji?
 
Kwani tatizo letu kuu ni uzalishaji mdogo wa maji mtamboni, au ni uchakavu wa mabomba yanayoshindwa kufikisha maji yaliyopo kwa mwananchi?
Shida ni miundombinu sio uzalishaji, when wataamka na kujifunza
 
Walete wawekezaji hao, sisi tubakie kuwa walaji tu, kuzalisha na kuendesha miradi tumechemka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…