Korea Kusini yapiga marufuku ulaji wa Mbwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesema kuwa muda sahihi umefika wa kupiga marufuku ulaji wa mbwa katika nchi hiyo.

Rais Moon ambaye ni Moja ya watu wanaopenda ufugaji wa mbwa amesema upigaji marufuku wa ulaji wa mbwa ni njia mojawapo itakayosaidia kulinda wanyama hao wasiteketee zaidi wasiteketee zaidi

Hata hivyo inasemekana kuwa ulaji wa nyama ya mbwa umeshuka ingawa bado takribani mbwa milioni moja wanachinjwa kwa mwaka.

Nchi ya Korea Kusini tayari imepiga marufuku uchinjani wa kikatili wa mbwa na paka ilaulaji wa nyama hizo haukuwahi kupigwa marufuku.
 
... wamekosa hata nguruwe hadi wale mbwa na paka? Baharini huko vimejaa kila aina ya vilivyohalalishwa why mbwa na mapaka? Rais Moon Jae-in ni mkristo nadhani ndio maana ameanza mchakato wa kuharamisha mbwa na mapaka kuliwa kama chakula!
 
Ukiona watu wanautamaduni wa kula wanyama wa ajabu kama mbwa na paka jua kuwa kihistoria walikuwa maskini sana na maeneo yao hakukuwa na wanyama kama ng'ombe, mbuzi etc.

Mtu aliyezungukwa na ng'ombe na mbuzi hawezi kula mbwa.
 
Unawazungumziaje wahehe/wanyaru kule Iringa mkuu..?! Na wafipa wanakulaga panya huko Swax vp nao...?
 
... wamekosa hata nguruwe hadi wale mbwa na paka? Baharini huko vimejaa kila aina ya vilivyohalalishwa why mbwa na mapaka? Rais Moon Jae-in ni mkristo nadhani ndio maana ameanza mchakato wa kuharamisha mbwa na mapaka kuliwa kama chakula!
Kwani Iringa sio wakristo
 
Siyo kweli. Ni utamaduni km utamaduni mwingine na siyo umasikini. Mbona wamasai hawali samaki?
Nenda karatu vijijini huko kwa wairaq na wamang'ati. Ni masikini lkn hawali mbwa.
Ukiona watu wanautamaduni wa kula wanyama wa ajabu kama mbwa na paka jua kuwa kihistoria walikuwa maskini sana na maeneo yao hakukuwa na wanyama kama ng'ombe, mbuzi etc.

Mtu aliyezungukwa na ng'ombe na mbuzi hawezi kula mbwa.
 
Kwahiyo kwa sababu yeye anapenda ufugaji wa mbwa ndio anazuia watu wasile mbwa?

Eti, Ikitokea anapenda ufugaji wa kuku, Ng'ombe nk, hapo pia atapiga marufuku !!!? 🤣
 
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesema kuwa muda sahihi umefika wa kupiga marufuku ulaji wa mbwa katika nchi hiyo.

Rais Moon ambaye ni Moja ya watu wanaopenda ufugaji wa mbwa amesema upigaji marufuku wa ulaji wa mbwa ni njia mojawapo itakayosaidia kulinda wanyama hao wasiteketee zaidi wasiteketee zaidi

Hata hivyo inasemekana kuwa ulaji wa nyama ya mbwa umeshuka ingawa bado takribani mbwa milioni moja wanachinjwa kwa mwaka.

Nchi ya Korea Kusini tayari imepiga marufuku uchinjani wa kikatili wa mbwa na paka ilaulaji wa nyama hizo haukuwahi kupigwa marufuku.
Mbwa wanachinjwa kikatili sana
 
Back
Top Bottom