Mkuu unataka ujenge mwenyewe?
Korido ya kupita watu wawili mkapishana na inayoruhusu kupitisha mizigo kadha wa kadha inaanzia mita 1
ukubwa wa Sebule inategemeana na idadi ya watumiaji kama ni 5
Basi mita 5 kwa mita 4.5 inatosha ,Dinning ikiwa na mita 3 kwa mita 3 yafaa na Chumba kikiwa na mita 3 kwa 3m kinafaa
Mlango urefu unafunguka tu ni kuanzia mita 2.1
Madirisha yanatofautiana urefu kulingana na eneo lililopo
Sebuleni yanaanzia mita 0.5 kutoka sakafu na kwenda mpaka 2.4m (wastani wa 1.9m)
Urefu wa nyumba unaanzia mita 3 mpaka mita 3.5
Ngazi upana huanzia mita 1 na kimwuniko kile ni inchi 6 (150mm) na kikanyagio ni inchi 12 (300mm)
Ukihitaji Ramani ya makazi yako usisite kunijuza