Pre GE2025 Korogwe: Wananchi wataka vikwazo vya ushiriki mdogo chaguzi za 2019 na 2020 vishughulikiwe kuongeza ushiriki chaguzi za 2024 na 2025

Pre GE2025 Korogwe: Wananchi wataka vikwazo vya ushiriki mdogo chaguzi za 2019 na 2020 vishughulikiwe kuongeza ushiriki chaguzi za 2024 na 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000

Matukio ya wagombea kudaiwa kutoa rushwa, kukosekana kwa elimu ya uchaguzi na kutoaminiwa kwa baadhi ya wagombea na wananchi, kumechangia ushiriki hafifu wa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu uchaguzi wa mwaka 2019 wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Hayo yamebainishwa wakati wa uwasilishaji wa matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali la Tree of Hope kwa kushirikiana na Taasisi ya Wajibu Maendeleo yetu project ambapo katika vijiji vya Hale, Makuyuni na Kwashemshi vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Mkoani Tanga ni miongoni ya maeneo ambayo wananchi wake hawajajitokeza.

Kupata habari za mikoa yote kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa soma hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo katika kikao cha wadau wa uchaguzi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Ofisa Mradi Mwandamizi wa shirika la Tree of Hope mkoani Tanga Godluck Malilo Korogwe ni moja ya maeneo ambayo yalikuwa na ushiriki hafifu, kwa mujibu wa ripoti ya uchaguzi ya mwaka 2019.

Miongoni mwa washiriki Kutoka katika vijiji vya Kwashemshi, Mariam Amani amesema wao kama wanawake changamoto kubwa inayowakabili ni kukosa muda wa kupata elimu ya umuhimu wa kushiriki semina za kushiriki mambo ya uchaguzi.

Aidha mkazi wa Hale Salimu Ramadhani amesema elimu yakutosha itolewe kwa makundi yote hasa kwa wanawake na vijana huku wakianisha sababu za kutojitokeza ikiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuonekana kuwa hawawezi kuongoza kutokana na mtazamo hasi wa jamii kuhusu makundi hayo.

Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe Mwanaamina Mruma amesema watahakikisha wanafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye uchaguzi uliopita kwa kufanya hamasa ya uchaguzi kwa Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
 
Back
Top Bottom