Korosho Mtwara mnada wa leo 21/10/2022 kaa la moto kwa mkulima

Korosho Mtwara mnada wa leo 21/10/2022 kaa la moto kwa mkulima

mwanagezi

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2021
Posts
285
Reaction score
439
Ni baada ya Leo wakulima kugoma kuuza korosho za kwao kutokana na kutoridhishwa na soko la siku ya kwanza ya mnada. Bei ya juu ni 2000/=na bei ya chini ni 1590/=.

Hii siyo sawa kabisa na ukilinganisha gharama za uzalishaji kwa mwaka huu 22/23 kupanda kwa bei ya mafuta ya kupulizia na kumlipa mpuliziaji hili zao linataka kuleta ukorofi wa miaka Saba nyuma, watu wapeana hasara kwa kunguziwa vitu vyao na hasara nyingine za namna hiyo.
 
Kila mbuzi ale kulingana na urefu wa kamba yake na kila mtu atakula alikopeleka mboga
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni sio haki kuuza korosho 2000 ukilinganisha na gharama zinazotumika kuzalisha zao hili. Gharama za maisha zimepanda mafuta bei juu, mchele bei juu, unga bei juu nakadhalika lakini bei ya zao hili inazidi kuanguka msimu hadi msimu.

Ni nani atasikia kilio cha mkulima, ni lini mkulima atafaidika na zao hili. Zao kubwa kama hili tulitegemea limuinue mkulima cha ajabu lina mkandamiza mkulima kwakuwa na gharama kubwa za uzalishaji na mauzo finyu huku wakifaidika wachache na matozo yao.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni sio haki kuuza korosho 2000 ukilinganisha na gharama zinazotumika kuzalisha zao hili. Gharama za maisha zimepanda mafuta bei juu, mchele bei juu, unga bei juu nakadhalika lakini bei ya zao hili inazidi kuanguka msimu hadi msimu.

Ni nani atasikia kilio cha mkulima, ni lini mkulima atafaidika na zao hili. Zao kubwa kama hili tulitegemea limuinue mkulima cha ajabu lina mkandamiza mkulima kwakuwa na gharama kubwa za uzalishaji na mauzo finyu huku wakifaidika wachache na matozo yao.
Kabisa hii siyo sawa maana ukitoa ushuru wa baadhi ya vibali mkulima anaweza pata 1470/=sasa huyu alikopa dawa, aliweka vibarua kulimia shamba na gharama za namna hiyo.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Kumlipa mkulima bei ya tsh 2000 na sawa na kumrudishia gharama yake bila kujali katumia muda gani shambani na vilevle bila kujali gharama za maisha zimepanda, KWELI UBINADAMU KAZ.

Hebu tujiulize swali dogo sana, kilo moja ya unga kwa sasa ni tsh 1800, mchele tsh 2400, kuna haja ya kureview minada ya korosho na kuwa na bei elekezi(dira) hakuna mnada duniani unapigwa bila kuwa na bei dira.

Watu wanakopa mabank na kuingiza kwenye kilimo ili kilimo kiwe na tija but unakuta wanaosimamia ndio mabosi, ifikie hatua kama vyama vya msingi haviwezi kuwa na maamuzi na hili, wakulima wazalishe korosho then kila mtu ajue atauza wap coz huu sio uungwana, mfano ukienda supermarkets yeyote ile unapata korosho iliyoandaliwa nusu kilo kwa tsh 10000 namaanisha uandaaji wake wala haufikii elfu tano so kama tatizo halina ufumbuzi kila mkulima aruhusiwe kufanya biashara atakavyoweza kila mtu ana matatzo yake so asionekane mtu anayo makubwa kuliko ya mwenzake. Very sad kwa wakulima poleni watu wa kusini, ila msipo amka mataendelea kulalamika.
 
Kumlipa mkulima beinya tsh 2000 na sawa na kumrudishia gharama yake bila kujali katumia muda gan shambani na vilevle bila kujali,gharama za maisha zimepanda,KWELI UBINADAMU KAZ,Hebu tujiulize swali dogo sana,kilo moja ya unga kwa sasa ni tsh 1800,mchele tsh 2400,kunahaja ya kureview minada ya korosho na kuwa na bei elekezi(dira) hakuna mnada duniani unapigwa bila kua na bei dira.

Watu wanakopa mabank na kuingiza kwenye kilimo ili kilimo kiwe na tija but unakuta wanaosimamia ndio mabosi,ifikie hatua kama vyama vya msingi haviwezi kuwa na maamuzi na hili,wakulima wazalishe korosho then kila mtu ajue atauza wap coz huu sio uungwana,mfano ukienda supermarkets yeyote ile unapata korosho iliyoandaliwa nusu kilo kwa tsh10000 namaanisha uandaaji wake wala haufikii elfu tano so kama tatizo halina ufumbuzi kila mkulima aruhusiwe kufanya biashara atakavyoweza kila mtu anamatatzo yake so asionekane mtu anayo makubwa kuliko ya mwenzake. Very sad kwa wakulima poleni watu wa kusini,ila msipo amka mataendelea kulalamika.
Ni kazi sana.
 
Yaani hapo hiyo 2000 bado kuna makato kama 200 na chenga chenga hivi watu wa kangomba kilio
 
Back
Top Bottom