mbj
Member
- Jun 24, 2013
- 39
- 44
Hii ilikua imebakia historia lakini sijui kitaalamu historia ikijirudia inaitwaje. Ifikie hatua watu wapewa kilicho chao, laiti kama pangekua na chaguo la namna watu wangepata riziki zao nadhani wangechagua. Kwa jinsi korosho zinavyogharamisha wakulima, isingetokea mtu kuwaletea bei ya kokoto ndoo moja ndogo.
Watu wanahangaika mwaka mzima kutimiza malengo yao lakini utaratibu unavyokuja inatoa machozi. Embu fikiria mnada wa kwanza unakuja na bei ya Tsh 2,000, wa pili na wa tatu itakuaje?
Wakat huo huo kodi kwa mkulima imepanda mpaka 310 kwa kilo moja kwa madai ya kupanda kwa gharama za uendeshaji. Bila kujali kuwa gharama za maisha zimepanda zaidi ya mlima Kilimanjaro.
Watu wasigomee mnada kwa kipi kilichowardhisha? Jamani ipo siku kama watu hawatapaza sauti zao basi kuna watakao wasaidia kupaza sauti na zikasikika. Ukila kwa urefu wa kamba yako sawa lakini hata ng'ombe anapokamuliwa bila kupewa malisho hakika utamkamua damu, na wakati utakapohitaji maziwa tena wala hakuna utakachopata.
Watu wanajijua hawana cha kuwafanya lakini walau wapeni chenye tija ili wakati ujao muweze kupata kingine. Tanzania ni nchi ya amani sana, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.