Korosho yageuka bomu kwa wakulima

mbj

Member
Joined
Jun 24, 2013
Posts
39
Reaction score
44
Hii ilikua imebakia historia lakini sijui kitaalamu historia ikijirudia inaitwaje. Ifikie hatua watu wapewa kilicho chao, laiti kama pangekua na chaguo la namna watu wangepata riziki zao nadhani wangechagua. Kwa jinsi korosho zinavyogharamisha wakulima, isingetokea mtu kuwaletea bei ya kokoto ndoo moja ndogo.

Watu wanahangaika mwaka mzima kutimiza malengo yao lakini utaratibu unavyokuja inatoa machozi. Embu fikiria mnada wa kwanza unakuja na bei ya Tsh 2,000, wa pili na wa tatu itakuaje?

Wakat huo huo kodi kwa mkulima imepanda mpaka 310 kwa kilo moja kwa madai ya kupanda kwa gharama za uendeshaji. Bila kujali kuwa gharama za maisha zimepanda zaidi ya mlima Kilimanjaro.

Watu wasigomee mnada kwa kipi kilichowardhisha? Jamani ipo siku kama watu hawatapaza sauti zao basi kuna watakao wasaidia kupaza sauti na zikasikika. Ukila kwa urefu wa kamba yako sawa lakini hata ng'ombe anapokamuliwa bila kupewa malisho hakika utamkamua damu, na wakati utakapohitaji maziwa tena wala hakuna utakachopata.

Watu wanajijua hawana cha kuwafanya lakini walau wapeni chenye tija ili wakati ujao muweze kupata kingine. Tanzania ni nchi ya amani sana, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
 
Nchi ya amani au ya Utulivu?Kuna amani hapa!!?mtu anaishi maisha hajui leo atakula nini,awe na amani?Nani wa kuja kuwasemea kama nyie hamjitambui,ni viongozi wangapi wamejaribu kuwasemea lakini ,wazee wa propaganda wanawaambia kuwa hao wanao waamusha kujua haki zenu hawaitakii nchi mema,na kweli mnakubaliana nao?!!Yaani myonywaji anaungana na mnyonjwaji kumpiga vita mtetezi.Leo hata bei ya unga ifike 3000!!huwezi kumuona mnyonge anapika kelele hadharani,atakachosema ,ni mipango ya Mungu.
 
Hili la stakabadhi ghalani naona limeshaferi.

Hao wanunuzi nao ni cartel ya kumuumiza mkulima..hakika mkulima wa nchi hii ni kaanyagio la wanasiasa na wafanyabiashara.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tena hiyo 2000 utakuta kampuni inataka tani 10 kwa bei hiyo lakini mzigo mkubwa kama tani laki moja utakuta kampuni inanunua kwa 1480. Hapo bado makato.


Hakika kama hali ikiendelea hivi, uzalishaji utashuka mno huko mbeleni maana wakulima wengi watakosa fedha za kutosha za kununulia pembejeo, mbolea, gharama za kulimia shamba, kupalilia, kupulizia, kukonyoa n.k.
 
Na mazao ya ndani kwa sasa tunashindana kununua na Kenya huko! Sasa Ksh ukilinganisha na Tsh, utagundua mpaka tukifika Xmass, angalau kundi la kati litakuwa limepungua au kuisha kabisa.

Ama tajiri au Fukara
 
Mtanikumbuka
 
Demand and Supply ndio inaamua bei ya soko.
Ni rahisi sana kuongea ya kwenye vitabu ila uhalisia unabakia palepale,unadhani demand ya unga wa mahindi kwa sasa imeongezeka kuliko supply?Ukiongea kutoa mawazo yako hii haikatazwi but reality haijawahi kufichwa ni kama jua,ikiwa hapahapa tz korosho iliyochakatwa inauzwa kilo moja kwa elfu 20000 unaniambiaje hapo mizani ya demand and supply ielemee upande mmoja,labda tuangalie angle nyingine na sio uhitaji kua mdogo,
 
Mkuu hizo ni principle za uchumi ,demand and supply ndio inaamua bei ya soko!! Kama Supply ikiwa kubwa mtaani lazima bei ishuke ,ukiona bei imepanda maana yake supply ni ndogo kwenye soko....Kwenye issue ya korosho ebu angalia shida ni nini hapo kwenye demand and supply na pia kuna kitu kinaitwa Free Market Economy sio lazima uiuzie serikali korosho ,tafuta soko kwa bei unayoitaka wewe wanunuzi wapo!! Waveti wananunua sana Korosho.
 
Now your demand kwenye soko la korosho ni kubwa sana,ninaposema hvyo namaanisha uzalishaji wa korosho ni mdogo sana ikilinganishwa na mazao mengine ya biashara after all ilitakiwa kuwepo na free market economy ili tuheshimiane,unajua inauma kwa mkulima asiyeyajua haya tunayoyaongea,mwisho wa siku akimaliza kuuza anaenda kununua korosho nusu kilo ambazo zimepakiwa kwa tsh 10000 so from their unaweza kurudi kwenye demand and supply afu ukachakata tena,kwa simple mathematics kilo moja kilo 100 ya korosho ghafi unatoa korosho kilo 36 mpaka 40 zilizochakatwa kwa kilo moja ni tsh 20000 so kama ni free market economy mkulima ni mtu wa kufurahi after mavuno na sio kwa kulalamikakila ikifikia kuuza mazao yake,fanya research nenda kanunue korosho in any market uje na bei yake,
 
Kwenye soko la korosho ghafi Kwa India bei ni zaidi TSH 3000, India ni moja ya soko la korosho la TZ.


kiuharisia kwenye hii biashara hakuna free market principles, wanunuaji wameunda carter na kupanga bei ya kununulia wakilenga faida ya zaidi ya 50%, Kwa sasa hata mitandao ya simu imeunda carter za kupanga bei za bando hawashindani tena
 
Tatizo wanasiasa Wetu na viongozi wetu wameingia kweny hii biashara yan hiz kampun zote ni zao wakulima sis ndo tunazugwa na zilizobak shamba bora tubangue
 
Kuna wakati kulikuwa na bei elekezi, hivi ilifutwa na nani kwenye korosho
 
Kama bei ya mnada ni 2000 itakuwa jau sana.maana kuna watu wananunua 1400 hadi 1500 hapo bado gharama nyingine kuzikausha na kuzirudisha ndani na hapo kila kilo 1000 lazima kilo 100 ikate, kwa wafanya biashara pia hawatapata hela kiivyo .hii ishaanza kuwa biashara kichaaaa.......!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…