Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
USIOMBE YAKUKUTE WE KAPUKU
SEGEDANC YAKO
Korti yamwachia mtoto wa Keenja
na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana ilimwachiria huru mtoto wa mbunge wa Jimbo la Ubungo, Charles Keenja, Eliasa Keenja, na wenzake watatu baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.
Mbali na Keenja washtakiwa wengine waliofutiwa kesi ni Ahmed Mbilinga (Meneja wa NHC, Mkoa wa Tabora), Frola Nhamkolomwa na Damas Ngoiya ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 300.
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa, alisema amefikia hatua ya kuwaachiria huru washtakiwa kwa sababu ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umeshindwa kuishawishi mahakama kuwaona washtakiwa hao wana kesi ya kujibu.
Alisema ushahidi uliotolewa hauwezi kuwatia hatiani kwa kuwa hauonyeshi kama kweli washtakiwa hao walivunja nyumba ya mpangaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Li Jinglan, na kuiba vitu hivyo.
Awali, washtakiwa hao walidaiwa kuwa Mei 9, 2006, katika eneo la Kinondoni, Dar es Salaam, waliingia kwenye nyumba ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) anamoishi, Li Jinglan, na kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 300.