Kosa la huyu mwanaume ni nini?

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
17,216
Reaction score
26,225
Kuna jamaa yangu/rafiki yangu kipenzi ana hali ngumu nyumbani kwake ikanibidi niamue kuingia JF kusaka msaada wa ki-mawazo,ijumaa jioni jamaa alipotoka kazini alipitia sehemu akapata Bia zake tatu hivyo mpaka anainingia nyumbani iilikuwa kwenye saa mbili na nusu,alipoingia akasalimiana na mkewe akaenda kuoga then akarudi sitting room akimsubiri mkewe amuite kwenye meza tayari kwa chakula,ghafla ikawa kinyume aliyekuja kumuita ni House girl wake, baada ya kumuambia chakula tayari wakati akiondoka yule jamaa akamwambia "siku hizi unanenepa" yule H/girl hakujibu kitu,kumbe mama watoto kamsikia,yaani ugomvi uliozuka hapo mpaka leo hii hawaongei,sasa waungwana wa JF huyu jamaa kakosea wapi?
 
Pole sana ila hajakosea kiviiile..
Wivu tu wa kike wa mama watoto...
Ni upepo tu yataisha....
 

Hajakosea sasa kama Housegirl anapendeza asisfiwe
 
kaoa mtoto, na wakati anaoa alijua hayo, hivyo basi hana budi kumlea mpaka akue kama yeye ili waendane, na utoto sio umri tu bwana, hata kukomaa kimawazo na busara ni muhimu, na hii ndio shida watu wanataka kuoa warembo tu wenye umri mdogo/hawajapevuka kiakili, leeni sasa mpaka wakuo pumbavu nyie, wakati mnaoa hamkutaka ushauri, sasa ndo mwasumbua, leeni mtoto huyo akue ...


 
Reactions: LD
kunenepa sio sifa. wanawake wengi ukiwaambia wamenenepa wanakasirika...sasa huyo mama sijui kwa nini amemaindi labda kama anajua mumewe anapenda wanawake wanene
 
Mi nngekuw huy mmama hat nsinge-mynd,mana cpend unene n hat ctishikag wen my bf akiw amesimam o kumwangalia big fatty assy women!
 
kwa mume wa mtu kumsifia housgirl kuhusu maungo yake ni utovu wa nidhamu na ni kiashirio kikubwa kuwa ameanza kumtamani.
 
kunenepa sio sifa. wanawake wengi ukiwaambia wamenenepa wanakasirika...sasa huyo mama sijui kwa nini amemaindi labda kama anajua mumewe anapenda wanawake wanene
si kila mwanamume anapenda mwanamke mwembamba japo simjui huyu mwanamume lakini tayari ameonekana kuanza kumtamani hg wake.
 
Mbona fresh tuu.. Ila shida inakuja endapo tuu huyo jamaa hana tabia ya kumsifia na mkewe pia.
 
Unene wa house gal yeye wamuhusu nini
Acha anuniwe
OTIS
 
Hivi hapo kamsifia au katoa tu taarifa kwamba na yeye ameshagundua kwamba h/geli kanenepa kuliko zamani?
 
hapa tatizo ni kubwa sana......
kama ni mimi mkewe....nahama nyumbani.....
mwanaume maalun kweli huyo.......

Preta taratibu
mambo haya mnayalea wenyewe
we mke umekaa jikoni huko unafanya mambo yako au sijui uko wapi unamuachia house gal kuja kuniitia chakula
Sifa nitatoa kwake maana ungekuja mwenyewe ningekupa hiyo sifa wewe na wala nisingemuona house gal kuwa kanenepa
Hapo na akija kesho yake namwambia tena duh una mwanya mzuri hata kama hanao ili uzidi kupasuka
Mnawapa air time wenyewe wakiingia hewani mnaaanza kulalamika
(sorry kuna mtu kaiba paswedi yangu hapa )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…