Kosa la kumuuza Dani Alves bila kutafuta mbadala wake

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Dani Alves akiwa kama mchezaji wa Barcelona Fc akicheza nafasi ya Beki mbili na kuuzwa msimu huu kwa Vibibi kizee vya Turin(Juventus),alikua na mchango mkubwa sana pale barcelona.

Kutokana na mfumo wa Barcelona wakati mwingine kutumia beki 2 na 3 kushambulia Dani Alves alifiti sana kwenye Mfumo na kuisadia Barcelona Fc kuchukua karibu makombe yote muhimu na pia wakati mwingine yeye mwenyewe kufunga kutokana na umahiri wake wa kushambulia kwa kasi na pia kupiga mashuti makali.

Tangu Ameondoka Upande wa kulia wa Barcelona Umepwaya sana pamoja na kumchezesha kinda wao Sergi Robert bado hana vile vitu vya Dani Alves pia bado uzoefu wake kwa mechi kubwa sio mzuri

Barcelona wanahitaji kusajili beki mbili mapema kabla mambo hayajawaendea mrama zaidi

Je ni beki mbili gani kwa sasa anaweza kuingia kwenye mfumo wa soka la Barcelona na kuziba nafasi ya Dani Alves kwa Ufasaha?
 
Ukiona nashabikia barcelona jua ana cheza na Arsenal au Simba.

Kwa hiyo wakiwa hawaeleweki ndio nafurahi
 
Ukiona nashabikia barcelona jua ana cheza na Arsenal au Simba.

Kwa hiyo wakiwa hawaeleweki ndio nafurahi
tukko kwenye mpango wa kurekebisha hiyo kona. Vidal kashindwa kazi. tutakuwa kama katyusha kwenye offensive, unazipata katyusha?

Reactions: PNC
Target yao ilikuwa Hector Belarin wa Asernal sijui imeishia wapi.
 
Mistake ya juzi ya sergi Roberto ilikuwa ya kawaida ,so far amekuwa vzr ana assist 4

Ttz ya Barca playmaker ,rakitic siyo mzr kwenye kuchezesha na kuhold mipira ..iniesta pekee ndiye nguzo master plan pale kati ,,,Barca saizi kwenye kiungo hawapo strong kihivyo rahisi sana kupotea ..iniesta muhimu ,type ya xavi iletwe pale ..verratti hata coutinho..fullback sijaona pengo sana
 
Tatizo lako wewe unajifanya unaijua sana FC Barcelona, kumbe hujui lolote .. Embu thibitisha kama kweli Dani Alves aliuzwa kama uzi wako unavyodai!

Kwa taarifa yako tu " Dani Alves hakuuzwa bali aliamua kuondoka mwenyewe baada ya kumaliza mkataba wake".
 
Joa cancelo winga na fullback wa Valencia anahusishwa sana na hata last summer alihusishwa sana

Yupo vzr kwenye dribbling, pace nk
Kama ulitizama game ya Barca vs Valencia alimsumbua sana Digne
 
thanks kwa correction Ndugu,sijui lolote ok njoo wewe mwenye kujua umwagw vitu nahisi hata spelling za neno Barcelona nimekosea.

Una hisa pale nini Ndugu?
 
Joa cancelo winga na fullback wa Valencia anahusishwa sana na hata last summer alihusishwa sana

Yupo vzr kwenye dribbling, pace nk
Kama ulitizama game ya Barca vs Valencia alimsumbua sana Digne
kama sikosei game na Mancity Marcherano alipiga Mbili kabla pique hajaumia

wanahitaji kuvuja banki wanunue beki mbili nasikia wako na mpango pia na yule wa PGS Sergi Aurier/Ivory coast
 
thanks kwa correction Ndugu,sijui lolote ok njoo wewe mwenye kujua umwagw vitu nahisi hata spelling za neno Barcelona nimekosea.

Una hisa pale nini Ndugu?
Ili tuondoe sintofahamu itapendeza kama utataja timu unayoshabikia ili tuende sawa.. Binafsi naamini katika SIMBA SC (Taifa Kubwa) & FC Barcelona..
 
tukko kwenye mpango wa kurekebisha hiyo kona. Vidal kashindwa kazi. tutakuwa kama katyusha kwenye offensive, unazipata katyusha?

daa Arsenal atapona sasa kwa izo kombora/Katyusha[emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Target yao ilikuwa Hector Belarin wa Asernal sijui imeishia wapi.
Dogo alisema akipigiwa simu toka Barcelona hapokei nahisi kajifunza kutoka kwa

Alex Song
Fabregas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…