Ni kijana aliejaaliwa kuwa na familia yake mke mzuri na watoto wawili, miaka kadhaa imepita alikua kwenye mahusiano na binti mmoja walipendana ila bahati mbaya uhusiano uliisha hawakuweza kuoana kwa sababu ya tofauti ya dini zao kila mmoja akiwa na imani kali kwa dini yake. Kila mmoja alimbembeleza mwenzie amfate dini yake ikashindikana basi wakaachana kwa heri na kubaki marafiki.
Baada ya muda kupita kijana kapata mwanamke wa dini yake,wakafunga ndoa, lakini mawasiliano na yule x hayakuisha. Mdada akiwa na shida jamaa yupo kwa ajili yake anamsaidia. Mwanaume alikua kijana safi katika ndoa yake hakumsaliti kwa kufanya kitu kibaya, hata x hakuwa akimla ni mawasiliano na kumsaidia shida zake.
Ilipita miaka mitano, siku moja x akamuomba waonane ana shida sana, kijana kwa mara ya kwanza akaenda kumsikiliza, kamkuta dada kajiweka na kanga moko huku msambwanda ukijidhihirisha kuwa dunia ni duara, shetani ana nguvu kuliko break down, kanga ikadondoshwa kaka kala mzigo karudi kwake.
Baada ya miezi kupita, x kavunja ukimya hesabu zake zikiwa tayari muda huo jamaa atakua kala sana nyumbani, akatuma msg kwa wife nendeni mkapime afya, zimepita siku kupima jamaa kaukwaa, miaka mitano yooote x anapanga revenge tu ilhali waliachana poa.
Nawakumbusha microwave wapasha viporo, usione kutunukuwa ukahisi kamiss pigo zako za kichina, we kuendelea na maisha mwenzio hayamuendei usidhani anafurahi. Alamsik!