Koti la Michael Jackson lauzwa mil 600/=

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
KOTI la kihistoria la Michael Jackson (MJ) limeuzwa katika mnada kwa Dola za Marekani 298,000 (zaidi ya Sh milioni 600) ikiwa ni mara tatu ya bei halisi ya koti hilo.

Koti hilo lililonunuliwa na mfanyabiashara mmoja tajiri kutoka Texas, ni lile jeusi lililovaliwa na MJ katika ziara yake ya Bad World Tour iliyokuwa ziara yake ya kwanza nje ya kundi, aliyoifanya mwaka 1987 mpaka 1989.

Imeelezwa kuwa mbali na mfanyabiashara huyo kuchukua koti hilo lenye saini mgongoni isiyofutika iliyoandikwa na Michael, pia alinunua vitu vingine 100 vya kumbukumbu ya mfalme huyo wa muziki wa Pop aliyefariki mwaka 2009.

Hii ni mara ya pili kuuzwa kwa koti la MJ kwenye mnada. Mwaka 2011, koti lake maarufu lenye rangi nyekundu na nyeusi alilokuwa nalo kwenye video yake ya Thriller liliuzwa kwa dola milioni 1.8 (zaidi ya Sh bilioni 4.1).

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…