Kotukuamini dini haimaanishi siamini katika uwepo wa Mungu

Kotukuamini dini haimaanishi siamini katika uwepo wa Mungu

hitler2006

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2014
Posts
489
Reaction score
454
Kuna dhana imejengeka kwa watu wengi na sasa inaelekea kuwa ndo ilivyo
Utakutana na mtu akishakuuliza jina tu basi na jibu la imani yako anakua nalo!

Sasa kuna hawa wengine wanao amini kama humuabudu allah wala God/jesus wewe basi huna mungu.

Kiasili mwanadamu awaye yote yule ni lazima aabudu...sasa kuabudu ni hali ya kujishusha na kusurrender kwa mamlaka ya juu,iliyo juu ya upeo wa fikra zetu wanadamu. Ndiyo maana ni rahisi kukuta jamii haina shule wala zahanati lakini sehemu za madhabahu utazikuta.

Niwaambie ndugu zangu wakristo na waislamu kuwa si kila asiyeamini katika miungu yao basi ni mkana Mungu.

Idadi ya wakristo na waislamu duniani haizidi bil 3,na dunia ina watu wapatao bil 8.
imani ina nguvu
Imani inaponya
Imani inatenda
Dini inafitinisha
Dini inagawanya
Dini inaondoa amani(gaza na israel)
 
Dini ni njia ya kukufanya ufikie kwa MUNGU Ila ikuwa una uwezo wa kumfikia MUNGU pasipo dini itakuwa bora pia .
 
Ukweli mtupu, binafsi naona hizi dini ni chanzo cha migogoro, chuki kudharau wengine kwa kuamini dini yako ndio bora kuliko wengine na mengine mabaya....nipo tofauti na hayo.

Naamini katika amani, kupenda na kujali wengine, kusaidia pale uwezavyo, kila mtu ni sawa hakuna alie bora na mengine ya hivyo.

Hizo dini 👎👎
 
Imani ni uhakika wa mambo yajayo.

Mfano unapotoka home kwenda kazini unaamini utafika - faith

Ukiumwa unakunywa dawa unaamini utapona - faith

Watu wengi wanafikiri imani ipo kwenye dini tu, kumbe hata kuamka asubuhi kufanya zoezi ni Imani, pia!!

Kila mtu ana Imani, mtu aliyepoteza imani ni yule ambaye amekata tamaa ya Maisha, mara nyingi utaskia Fulani kajiua!!


Screenshot_20240927-073545.jpg
 
Back
Top Bottom