Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KUTOKA UWANJA WA MKAPA HADI UWANJA WA MWALIMU NYERERE NYOTA WA YANGA
Mwanangu Taufik ni mpenzi mkubwa wa Yanga na mimi ni Mnyama.
Kwa kweli nateseka sana maana baada ya zile hamsa yeye ni kunikumbusha kivumbi kilichotokea kwa Mkapa.
Juu ya haya yote ni mwana mwenye huruma ananisaidia kwa mengi khasa katika kwenda huku na huku.
"Baba wewe sasa mtu nzima barabara za Dar-es-Salaam huziwezi ukiwa na safari niite nikupeleke."
Kweli daladala na boda boda zimefanya barabara kuwa ngumu kuendesha kwa wazee kama mimi.
Basi anakuwa kwenye usukani na mimi pembeni yake.
Safari nzima nampa stori za zamani na yeye ananipa habari motomoto za Yanga na Simba lakini hana la kheri kwa Wekundu wa Msimbazi.
Nastahamili maana nikijitia kidomodomo nitakosa mengi.
Jana Bismillah kanipa taarifa ya mahojiano ya Aden Rage kuhusu mechi ya Simba Jumamosi ijayo na aliyosema kwenye FM Station moja.
Rage kawapongeza Yanga kwa muziki wake.
Hivi ndivyo anavyoniadhibu mwanangu huyu.
Si mmeona hapo pichani kanawekea uzi mkali wa Yanga?
Leo tulikuwa tunamsindikiza ndugu yake ndege ya usiku "reporting" time saa sita.
Nduguye ana "check in" na sisi na nduguze wengine tumekaa tunasubiri avuke kote ndiyo tuondoke mara kanigutua.
"Baba angalia kule unamuona yule na yule."
Nageuza shingo natazama.
Mastaa wa Dar Young Africans waliomkabidhi Belouizdad mvua nne kwa nunge.
"Wale ndiyo waliowatia kiwewe jamaa juzi goli nne nusra zifike tano."
Hii goli tano lazima aitaje ingawa Yanga walishinda goli nne.
Mwanangu hana huruma ananirejeshea kilio upya kunikumbusha goli tano za Kwa Mkapa.
Kwa kweli nimeangalia ile mechi na hakika Yanga ingefikisha goli tano na kilichowaponza hawa ndugu zetu ni kuvaa zile jezi nyekundu.
Yanga wanaona wanacheza na Simba.
Yanga walitandaza boli safi la kufurahisha nafsi lakini kwangu vilevile kunijaza hofu.
Si muda mrefu tutapambana na muziki ule.
Sitaki hata kuwaiza siku hiyo.
Sasa mwanangu na wenzake wamekwenda kuwaangalia hawa mastaa kwa karibu kisha wamerudi maskani.
Nawauliza, "Mmepiga picha?"
Hawana moja.
Lelelele, lelelele.
Uzee dawa.
Nawaambia, "Nyie mmefika hadi walipo hawa nyota wa Yanga mnaogopa kuwaomba kupiga picha na wao?"
Nilijua hawataweza kupata fursa kama ile hadi kiama.
Nikanyanyuka hadi walipokuwa vijana hawa wako kwenye foleni ya :ku-check in."
Kufika nikawatolea salamu na kuwapa mkono huku nawaambia, "Good football congratulations...can we have photos please!"
Wamefurahi wenyewe wamejipanga pembeni yangu.
Tukapata picha hii ya ukumbusho na nyingine nyingi.
Kushoto: Kouassi Attohaula Yao (Jeshi), Mohamed Said (Eusebio), Pacome Zou Zoua (Le Professeur) na Tawfiq Kazaliwa.