Wakati Kamala anamtukana Dr. Slaa kwamba ni Mbumbumbu, wakati wagombea Ubunge wa CCM wakimtukana Dr. Slaa juu ya Mahusiano yake akina Kova walikuwa Wanakenua Meno. Sasa Yamemkuta Mku wa Kaya mnaanza kuhangaika. Jana Hadija Kopa amemtuna Dr. Slaa Mkaendeea kukenua Meno huku mkiinua Vodole Juu kuitikia Mipasho ya Hadija Kopa
Akitunakwa Dr. Slaa poa tu kwa Sababu ametukana Mgombea wa Urais, Akitukanwa Kikwete ametukanwa Rais
Mkiwa Fair mtaheshimika ila mkiwa Biased hamtaheshimika
Tatizo la CCM hawajui impact ya yale wanayoyafanya, wakija kugundua wamekosea wanakuwa tayari wamechelewa na mambo yameharibika. Kusema ukweli hata kama watu walikuwa hawamfahamu huyo mgombea mbunge ndio sasa wamepta nafasi ya kumfahamu.
kilichosemwa si matusi, Kikwete kaambiwa hajafunzwa na mama yake, ooh yes atuthibitishie yeye kama amefuzwa na mama yake sio kutumia genge la maaskari kumsemea JK, NARUDIA , MGOMBEA WA CCM HAJAFUNZWA NA *****.
Kwa mtu makini na ambaye hafanyi kazi kwa kuambiwa na anafuata sheria basi siku ile pale Mwembeyanga angekamatwa mgombea ubunge pale pale,lakini kwa kuwa jeshi lapolisi lipo kisiasa zaidi kuliko kiutendaji na kufuata sheria za nchi ndio maana ilibidi wasubiri maelekezo toka kwa viongozi wa CCM na kuyatekeleza.
Nitafurahi sana kama kesi ikienda mahakamani maana ndio watanzania tutakapojua maana ya maneno ya kiswahili