Pole kwa kuwa njia panda.
Nakushauri utambue kuwa tunahitaji kusoma ili tuelimike, na tukielimika tutaweza kufanya chochote.
Aliyeelimika atatizama mazingira na atajua cha kufanya kwa namna ya elimu yake.
Najua mtu aliyekuwa askari na hana cheti cha ualimu lakini anapenda sana Physics, Chemistry na Hesabu lakini ameacha Uaskari na kuanza kufundisha tuition.
Na sasa ana tuition center kubwa sana Ukonga na anaingiza pesa nyingi bila stress za kukamata mwizi wala kulinda banks.
Tafakari mazingira yako kisha tumia elimu yako kujikwamua.
(Tukisomea kazi tunapata tusivyotegemea mbeleni)