impelle
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 832
- 1,107
Hbr ya wknd ndugu zangu
Niende moja kwa moja kwenye Lengo la kuandika uzi huu,
Nina mdogo wangu ni mhitimu wa kidato cha sita mwaka huu,alisoma combination ya HGL na kufanikiwa kupata matokeo mazuri ya daraja la kwanza la alama tisa.
Wakati najadiliana nae kutaka kujua anapenda kusoma nini na kuwa nani baadaye, nilishangaa kuona kwamba hajui kile anapenda kusomea shahada yake ya kwanza.
Leo nilikuwa napitia course mbalimbali mtandaoni,nikakutana na course moja ipo MZUMBE inaitwa Bachelor of Health system Management, kiukweli nimeipenda na nafikiri nikampe somo dogo juu ya hii course akielewa basi liwe chaguo la kwanza, ingine ambayo imesababisha niandike hapa kuomba msaada inaitwa SAFETY & OCCUPATION HEALTH hii naiona kuwa diversified sana ila sijui chuo gani kinatoa shahada yake na sifa za kujiunga.
Kwa kuwa napanga aombe vyuo vinne tofauti tofauti ili kuongeza nafasi ya kupata,naomba pia wana jamvi mnisaidie walau course nyingine nzuri ambazo mwanafunzi aliyesoma Arts atasoma na ikawa na future nzuri.
Ahsante