ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
KING RASHID ( K R MULLA) MSWAHILI ALIYETUKUKA TOKA TEMEKE ASIYE NA MAJINGAMBO TOKA KITAMBO...π₯π₯π₯π₯π₯π₯
_________________
Jina langu halisi naitwa Rashid Ziada , lakini
Jina langu la kisanii Naitwa "K R"
jina hili la K R lilitokana kwa Sababu sisi ndio tulikuwa waanzirishi wa Movement Ama harakati kwenye upande wa Muziki wa Rap tukiwa tunatokea mtaa wa Temeke jiji Da es salaam..
Kwa hiyo Mashabiki na wadau wa Muziki Mbalimbali kutoka Mtaa wa Temeke wakawa Wana Respect kile nilichokifanya katika Hii industry ya Muziki wa Rap nikiwa natokea Mtaa wa Temeke Enzi hizo..
Wananchi wa mtaa wa Temeke Wakawa wananiita kila Comer ninayopita " kaka Mkubwa"
Lakini jina langu halisi nililopewa na wazazi Wangu Naitwa " Rashid Ziada"
Kwa hiyo watu wakawa wananiita " kaka Rashid"
Mimi nikaamua kufupisha hilo jina la ( kaka Rashid)
Herufi K ilisimama kama ( kaka ) na Herufi ( R) ilisimama kama ( Rashid)
Kuanzia hapo nikaanza kutumia jina la " K R ".
π₯π₯π₯π₯π₯
Kuna nyakati hapo nyuma niliitumia majina kama vile "Eazy R & king Rashid"..
Lakini majina haya yalikuwa sio maarufu sana na wala hayakudumu sana midomoni mwa watu yakawa yamekufa...
Kuanzia
Hapo ndipo kila mdau na shabiki Yangu ndio wakawa wameanza kunipa majina mbalimbali kutokana na ushabiki wao " Ama mapenzi yao kwangu .
Mfano:
kr mulla ,Muziki mnene Cd 700, nk..
Haya Majina yalikuja Baada ya harakati kadhaa kufanyika kwenye Crew Tatu Ama Station Tatu (3)
G.w.m ( Gangster with Matatizo) , Wachuja nafaka , Tmk ..
Wachuja nafaka Ambapo lilikuwa ni Crew la watu wa Tatu (3)
Ambapo ni mimi KR , juma nature & dolo ilikuwa ni Mwaka 2001...
Wasanii & Crew ambazo zilikuwa zinaleta ushindani & battle kwenye Muziki Wetu Enzi hizo ni kama vile..
Niggas 2 rebulic , Da young Mobb, Kwanza Unit, W.w.A, Big doggy posse nk ..
Hizi ni sehemu ya Baadhi Tu ya majina ya Crew ambazo tulikuwa na Battle nazo kipindi hicho tukiwa kama Crew ya " Gangster with Matatizo ( G.W.M)..
Na kipindi hicho ilikuwa ni battle kweli kweli to Baina yetu sisi Gwm na Wao,
KWA hiyo ukipata chance kwenye stage ,
Ni lazima ujitume kweli kweli na sio Mchezo ..
Sehemu ambazo zilikuwa zinaandaa Matamasha & kupromote inshu za Muziki Ama zilikuwa ni sehemu za kukutania Wasanii Enzi hizo ni kama vile..
Coloniani culture, Rusiani Culture ( utamaduni wa korea & Urusi )
Empire, kumbi zile za kuonyesha Cenema ,..
Show zilikuwa zinaandaliwa kuanzia Asubuhi hadi jioni show Ama Tamasha linakwisha..
Lakini " Coco Beach " Beach party ndio angalau matamasha au show zao zilikuwa zinafanyika hadi Usiku wa Manane
Pool side ( kilimanjaro hotel) , hapa ilikuwepo swimming pool moja kubwa sana "
Watu wenye Uwezo wa kifedha & watu Maarufu Enzi hizo wao walikuwa na Desturi ya kukutana Eneo hili ..
Kuna Tukio moja ambalo siwezi kulisahau katika Maisha yangu nakumbuka Enzi hizo Tukio hilo lilitokea katika Viwanja hivyo vya " Coco beach" kwenye hayo matamasha ya " Beach β±οΈparty"
Crew yetu Enzi hizo ya " Gangster with
matatizo ( G.w.m)
Ikiwa imeundwa na wasanii kama....
Mimi Rashid ziada ( kr), Robert E. Makala ( D chief), Richard Makala ( Eazy Dope)
Eazy Dope & D chief ni ndugu ( mtu na kaka yake)
Moja Kati ya matukio siwezi kusahau
Ni siku ambayo sisi kama Crew ya Gangster with matatizo tulienda kufanya show ama kutoa Burudani Eneo hilo la Coco Beach ilikuwa ni mwaka 1998..
ambapo siku hiyo ya Tukio watu walikuwa wengi sana waliofanikiwa kuhudhuria katika Tamasha hilo..
Watu siku hiyo walikuwa na Vibe la hatari sana,( mapema tu)
hata kabla ya sisi wasanii hatujashika mic ( ilikuwa ni kwenye zile hatua za mwanzo za sound check)
Lakini sound cheki ilipokamilika mimi na Wezangu ( Gangster with matatizo)
tulipolifamia jukwaa ( stage)
Watu walipatwa na Vibe moja la hatari sana.
Mizuka ya kufa Mtu ..π₯π₯π₯π₯
Ikafikia hatua hadi watu wanashangilia Yaani!! Hisia zimewazidi Mashabiki mpaka wakapelekea Mashabiki kudondosha speaker zote ( system ya Muziki kwa ujumla katika lile jukwaa)..
Na kupelekea na party yenyewe kumalizika pale pale ( Muziki ukawa ume Turn off ) kutokana na vitu kudondoka..
Hii ilikuwa ni kali ya Mwaka lakini pia ni Tukio kubwa sana kuwahi kutokea katika Historia yangu upande wa mambo ya Burudani .
Mwaka huo huo 1998 Serikali ikawa imetoa Angizo & Tangazo Kwa Uongozi wa Clouds na mmliki wa Eneo lile na wananchi kwa ujumla kwamba kuanzia siku hiyo hakutakuwa na "Beach party" ikifanyika tena Eneo hilo lile la Coco beach..
Siku hiyo Vibe lilikuwa la hatari sana vibe lilikuwa kubwa kwa mashabiki hadi kupelekea uharibifu wa system ya muziki pale Coco beach..
Kiukweli katika safari yangu ya uimbaji Ama Muziki nilianzia kwenye mambo ya ku Dance " Break dance"
Nilikuwa nashiriki kwenye matamasha mbalimbali ya ku Dance Enzi hizo hadi mwaka 1989 - 90 ....
hapo ndipo Tukashawishika mimi na D chief kuingia kwenye ( Music Industry)
Muziki wa Hip hop ( Rap ) & Uimbaji baada ya kuwa kuna baadhi ya wasanii kutoka Ughaibuni Wame tu inspire kufanya Muziki...
Kipindi hicho kulikuwa hakuna Tv, Wasanii hao kutoka Mataifa ya Ughaibuni tulikuwa Tunafuatilia Kazi & Taarifa zao kupitia ( Magazine) kuna Brother mmoja alikuwa analetewa haya majarida ( Magazine )
Tukawa tunapata Taarifa za wasanii hao..
Wasanii kama Vile Ice Cube, Eazy E, na wasanii wengine tu wengi wa zamani Enzi hizo....
Ikapelekea sana Sisi kutamani kufanya Muziki.
Lakini pamoja na hivyo kuna Wezetu ambao walitutangulia katika Tasnia hii ya Muziki wa Bongo fleva kutoka Hapa Hapa Tanzania..
Makundi kama Kwanza Unit , lakini watu walio tu inspire kufanya Muziki kutoka Hapa Hapa Bongo ..
Kwa Upande wa wasanii aliye tu inspire ni msanii zavara mpojika " Chief ramsone " member wa Crew ya "Kwanza Unit". ..
Pamoja na Mc Eddy , ambae pia alikuwa ni member wa crew ya " kwanza unit" kwahiyo tukawa na Desturi ya kutembeleana mara kwa mara kwa kushauriana na kubadirishana Mawazo kipindi cha Weekend ....
Kwa hiyo wasanii hao walituweka karibu sana Enzi hizo walitufanya kama Wadogo zao katika sanaa ya "Muziki" lakini ki umri pia..
Na sisi kama G.w.m " Gangster with Matatizo"
Kuundwa Crew yetu ilikuwa ni Mwaka 1993 ..
Enzi hizo kila kijana alipenda kuvaa ki Gangster ( Gangster) kila kijana Enzi hizo ndio ilikuwa Anaona kama ni fashion ..
Hata style ya Mavazi ilijieleza " suruali kubwa , kofi , viatu vikubwa ..
Yaani kama wasanii wa Marekani style za mavazi ndio ilishika hatamu sana Enzi hizo ( T shirt π½ & π jeans)
π Nk ...
familia zetu zilikuwa ni sehemu ya familia zenye Maisha Duni( kiMasikini) . .
Changamoto nyingi tumepitia mimi Na D chief Enzi hizo katika harakati kibao za kusaka shilingi
Misoto kibao kwenye mambo ya prodution ( studio ) Nakumbuka kipindi hicho mimi na Mwezangu D chief Tulikuwa tunatembea kwa miguu kwenda studio kwenda kurekodi Enzi hizo..
Na vitu vingine kama hivyo ndio chanzo cha kupatikana hiyo idea ya jina & Neno " ( Matatizo)".
Kwa hiyo ni wahuni ( Gangster).....
..
ila wapo kwenye Maisha Duni ( lifestyle yao ya kimasikini)
Ndio maana halisi ya Neno Ama jina la Crew yetu ..
" Gangster with Matatizo" ( G.W.M)..
Kwa hiyo lilikuwa ni jina lenye uhalisia wa Maisha yetu ya kila siku Tulioishi Enzi hizo mtaa wa Temeke jijini Da es salaam..
Kwenye upande wa Crew yetu ya ( Gangster with Matatizo)..
Asilimia kubwa ya waandishi wa nyimbo katika Crew yetu nilifanya mimi na msanii D chief,....
sometime msanii D chief alikuwa anakuja na idea Yake ...
, Au mimi nakuja na Idea yangu ama tushare Idea mimi na Yenye tukikaa pamoja Gheto..
ilikuwa kama mtu mbili kama million mbili.. ( kr & D chief)
Hata Crew ya Gangwe Mobb imeibuka baada Yetu sisi..
kwa Maana wasanii kama vile ..
Juma nature , Inspector haroun, Temba, Daz baba , Luteni karama ,..
Nakumbuka Enzi hizo walikuwa wanakuja Nyumbani ( Gheto)..
tukawa tunawafundisha Namna ya Kuandika Mashairi A - Z na tuliwafundisha vitu vingi tu kuhusu Muziki (sanaa).
Baadae Maisha jinsi yanavyokwenda ikafika Muda ( nyakati kubadilika) .
tukawa nao humo humo kwenye kiwanda cha Muziki na tukaendelea kushirikiana nao kama Zamani wakati ndio wanaanza kujifunza Muziki..
Mimi kiukweli namshukuru Mungu kwakuwa nilibarikiwa kipaji cha kufahamu lugha ya kiswahili Vizuri ,..
nilikuwa Napenda sana lugha ya Kiswahili kwa hiyo kwenye inshu ya Uandishi ilikuwa jambo rahisi sana kwangu...
Kwa maana lugha uki hifahamu wala usumbuki kuandika Mashairi ..
Nilikuwa napenda kusikiliza na kufuatilia " "malega wetu " watunzi na waimbaji wa mashairi Enzi hizo , ...
ilikuwa ukifika Muda ( Saa saba mchana ) ..
lazima nifungulie kituo cha Radio Enzi hizo Radio ya Taifa " Radio Tanzania"
Kwenye mtaa wetu wa Temeke kiukweli sisi Gangster with matatizo baada ya kuanzisha Crew tuliweza kuwa inspire Vijana wengine kutamani kufanya Muziki pia,..
Na tuliweza kuifanya jamii ione kumbe kufanya Muziki inawezakana..
Hiki ndio chanzo cha kupelekea makundi mengi kuanzishwa mtaa wa Temeke..
Na kumbuka kwa kipindi hicho Temeke kiukweli Maisha ya watu ( wananchi)
Maisha yao yalikuwa ya shida sana ( umasikini)
Makundi Mengi yalipoanzishwa tukawa tunashirikiana nao kwenye kila hatua pale wanapohitaji ushiriki wetu kwao.
ila tulikuwa tukifika majukwaani ( stage). mbalimbali kwenye show kwenye Maeneo mbalimbali..
tulionekana kama Maadui ila baada ya show tunakuwa Marafiki...π₯π₯π₯
Na kumbukumbu kipindi hicho kulikuwa hakuna simu , kwahiyo promise ama mihadi tulikuwa tunapeana Baada ya show ama matamasha kumalizika..
Maybe tukutane " Coco Beach"
Na kipindi hicho wasanii wengi walikuwa wanakutana Coco Beach ..
Coco Beach & "salamada" mgahawa mmoja maarufu sana Enzi hizo ( ambapo kwa sasa lile Eneo ndio makao makuu ya kampuni ya GSM)
Hizi sehemu ikipita week ama Mwezi ujafika Maeneo hayo unakuwa umepitwa na vitu vingi sana katika Tasnia ya Burudani nchini Tanzania..
Project ya kwanza ya Gwm ( Gangster with Matatizo) ina historia kubwa sana ...
Siku hiyo Tulikuwa Tunaenda kurekodi na wakati ama kipindi hicho studio zilikuwa Chache,.
Kulikuwa na studio moja hivi Enzi hizo inaitwa " Mawingu Studio" ambayo ilikuwa ina milikiwa na Mr Joseph kusaga ,...
Kisa kilikuwa kama hivi..
sasa Siku hiyo tunakwenda kurekodi nyimbo yetu..
Tumetembea Toka tulipo kuwa Tunaishi Enzi hizo Mtaa wa Temeke hadi Mtaa wa Mwenge..
nakumbuka kipindi hicho hata Barabara ya kutoka hapa Veta karume haikuwepo kabisa ( kwa kifupi kulikuwa hamna Barabara)....
kulikuwa na makaburi tu .
Kwa hiyo tuli tokea mtaa wa Temeke hadi Mwenge kwa miguu...
Tukafika kule tukaelezwa kwamba Mr joseph kusaga hayupo ameenda "kitega Uchumi"
Mimi na Mwezangu msanii D chief safari ikaanza tukatoka Tena Mwenge baada ya kumkosa mr joseph kusaga hadi " kitega Uchumi ambapo tuliambiwa amekwenda...
Nashukuru Mungu
Tuka bahatika kumpata na akatueleza Mr joseph kusaga kwamba tuende siku fulani pale studio.."Mawingu studio"
studio ilikuwa mtaa wa Mwenge .
Tena tukaenda siku hiyo ,
Tukamkuta mr joseph kusaga hayupo pale studio ,..
wakatueleza ametoka kidogo kwahiyo tukarudi Tena nyumbani mtaa wa Temeke .
kama mara 3 hivi tukienda studio tunakuta Bado kurudi..
Toka Mtaa wa Temeke hadi mtaa Mwenge Bamaga ambapo ndio studio zilikuwepo...
Mwisho wa siku wale wafanyakazi wa pale studio wakatueleza njooni mida ya Saa kumi na moja jioni ..
Joseph kusaga boss wetu ndio atakuwa amerudi ,
Alipo rudi mr joseph kusaga ilimpindi amueleze producer wake " "Columba Mwingira" kwamba ebu ! ....
Wasikilize hawa vijana maana wamedai wao ni wasanii , na kama Kazi yao itakuwa zuri tufanye nao Kazi..
Na kama Kazi itakuwa mbovu tuwaeleze kwamba hapa amna nafasi ( waondoke)..
Na kumbuka kipindi hicho studio ya " Mawingu ilikuwa na producer mmoja anaitwa " dj bonnie luv" na Band yake ya " Mawingu Band "..
kwa hiyo hata producer "Columba Mwingira"
alikuwa ni A part of members wa " Mawingu Band"
Kwa hiyo producer "Columba" akawa amechukua jukumu la kurekodi Kazi yetu ya mwanzo kabisa tukiwa kama crew ya Gangster with matatizo na hiyo Ngoma inaitwa
" ki vyetu vyetu"
Alipoanza kurekodi producer "Columba" ghafla akapata vibe muda huo huo Akiwa ana Rekodi kutokana na Mashairi na style ya Uimbaji wetu ikamulazimu kwenda ofisi kwa boss wake Mr joseph kusaga..
Ili kwenda kumuita ili nae boss aweze kuja kutusikiliza ...
Alipofika nae Boss Mr joseph kusaga alipata vibe nae vile vile kupitia ushairi na zile punch za wimbo wetu ama project yetu ya kwanza inaitwa
" kivyetu vyetu "..
hadi kumpelekea boss joseph kusaga kufanya atununulie Chakula pamoja na vinywaji na ukumbuke siku hiyo tumeshinda bila kula siku nzima kwa hiyo tulikuwa tuna njaa hatari ..
Pamoja na uchovu & mchoko wa kutembea siku nzima toka Temeke hadi Tegeta....
Ilikuwa kama Saa 1 na nusu usiku ndio tuna maliza kurekodi Yaani ilikuwa ni Mwendo wa "One take"
Kauli ya joseph kusaga ilikuwa kama hivi
" vip ? Vijana mmeshakula Chakula ..
Mr Joseph kusaga Akapindi kutuma wafanyakazi wake pale " Mawingu studio"
Ebu!..
kawanunulieni Chakula hawa vijana ..
tukaletewa siku hiyo Chakula Aina ya chips & soda na nyama kama zote..
Kwa hiyo kuanzia hapo tukapata Utawala..
Mr joseph kusaga akatueleza Popote pale mkisikia show ama matamasha limeandaliwa na Clouds mnaruhusiwa kuingia Bure ..
Na kipindi hicho Alikuwa bado hajafungua kituo cha radio & tv..
Kipindi hicho Joseph kusaga na Wezake walikuwa ni waandaji wa disco sehemu moja inaitwa " continental" kilimanjaro hotel..
Ilikuwa ni hapo pamoja na kule mtaa wa Osterbey masaki ..
Joseph kusaga ndio akatuambia kuanzia leo na muda huu ma disco yote ya Clouds mtakuwa mnaingia bure ( free)..
Kwa upande wetu sisi kama Gangster with matatizo ikawa kama ni nafasi/ fursa ya kukutana na watu mbalimbali katika Tasnia hii ya Muziki wa Bongo fleva...
Na tukazidi kukomaa kimuziki ( sanaa)
kuanzia Hapo baada ya kupata support kutoka kwa joseph kusaga,
Album yetu ya kwanza ilikuwa inaitwa " mikosi"
Ngoma kama vile " yamenikuta"
Ilikuwa ni sehemu ya nyimbo zilizo kamilisha Album ya "mikosi"
na ukitazama kwa kipindi kile maisha yetu sisi wananchi wa mtaa wa Temeke & lifestyle yetu ilikuwa ya kimasikini Sana..
Verse yangu katika wimbo wa "yamemkuta" ft 2 proud ( mh Sugu)
Nilijikita kuzungumzia maisha ya uswahini Temeke..
"Yamenikuta mpaka najuta/ navuria bukta kibwebwe kwa mambo kedekede/ lakin kwa sasa ni mpweke sijui nicheke/ lakin nashindwa maisha ni ubingwa na mambo yamenitinga/ nginganginga maisha ni kama anakwenda anakwenda anaweka mpira/ ule kati linatokea varangati anapiga chenga moja mbili tatu anajaza kros/ lakin kwa sasa bongo jua la utosi hapendwi m2 linapendwa poch/ haha chacha kupe penda mzaha na vurugu2 mechi/ mbona hueleweki kula leki kufa hakuna bleki/ wewe usilete ..."
π₯π₯π₯π₯
Na kwa kipindi hicho wasanii wengi wa Temeke walikuwa Wana Desturi ya kutaja taja sana misosi na kwa sisi masikini inshu ya msosi ndio kulikuwa ni kipaumbele chetu cha kwanza kuliko vitu vingine vyote katika maisha yetu...
Tofauti na watoto wa kitajiri wao mara zote wanawaza starehe na kumbi mbalimbali za starehe mjini ...
Ila sisi wananchi wa Temeke maisha yetu ni magumu " msosi ndio kila kitu "
Inshu ya misemo Tata kwa sisi watu wa Temeke ni jambo la kawaida sana na mara zote msanii , hufanya muziki ama kuandika mashairi kutokana / kuendana na style ya maisha ya sehemu wanayotoka...
Na kila jamii au Eneo Huwa na misemo yake kwa kifupi ( culture) ya Eneo husika...
Culture yetu sisi watu wa Temeke ilikuwa ni ile misemo lakini sisi wenyewe tulikuwa tunafahamu tuna maanisha nini ..
mara nyingi tulikuwa tunapata maswali mengi sana kutoka kwa wale watu ambao sio wakazi wa mtaa wa Temeke maybe katika nyimbo Yako fulani....
ulizungumza neno fulani je?
Lina maana Gani?
Lakini kwa vijana ama wakazi wa Temeke tulikuwa tunaelewa Vizuri tu ..
Project ama Kazi yetu inaitwa " kamua" ft juma nature ..
Ilikuwa kama hivi .
Kama nilivyokueleza nyakati zile tulikuwa tayari na ukaribu na msanii juma nature Tangu zamani maana nimekueleza hapo nyuma kwamba juma nature ni sehemu ya wasanii ambao tulikuwa tunawafundisha muziki na vitu vingine kuhusu muziki kipindi cha nyuma.
Kwahiyo kumuomba juma nature kufanya nae Kazi ama project ya wimbo unaitwa " kamua " ilikuwa ni jambo rahisi maana Tayari tulikuwa ni marafiki toka zamani ..
Urafiki wa mimi na juma nature ulizidi kushika hatamu kupitia wimbo wake unaitwa " wimbi la njaa" hii project ilifanyika Bongo Records na kipindi hicho juma nature alikuwa hot ( alikuwa Tayari yupo chini ya Record label ya Bongo records)π₯π₯π₯
Na Tayari project nyingi hapa katikati tulishirikiana pamoja na juma nature na kupelekea kuundwa kwa crew wachuja nafaka Mwaka 2001 nk.. .
Nakumbuka mwaka 2003 Ile nyimbo ya " kamua zile Verse tuliandika mimi na msanii D chief
Kwa hiyo juma nature yenye tulimshirikisha kwenye kufanya Chorus tu ila vingine vyote tuliandika wenyewe..
Ikawa ni project ya Gangster with matatizo ft juma nature Ngoma inaitwa " kamua"
Na mimi kama K R nilifanya punch Ryhems za hatari kwenye Beat ya P funk majani ( Bongo Records)
Kuionyesha jamii kwamba Gwm ( Gangster with matatizo) tumerudi kwenye Main stream baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu..
Ndio maana kuna sehemu nimesema hivi katika hiyo Verse " gwm tumesharudi na mwaka huu lazima mavi ya .....chupi!!..
( Enjoy verse yangu katika wimbo huo wa " kamua).
"Akruu kunhaa yes p funk nipe beat kimakusudi Gwm mazimwi tumesharudi/ na mwaka huu lazma mavi ya gonge chupi/ wana niita kr mullah jibaba mziki mkubwa cd 700 njoo kichwa kichwa kula za uso saba/ huu ndio ujio ndio haina ufagio ni majitu ya mistar majabal yenye asili ya kimental na hisia kali/
mashairi ya mahangamizi/ kamua kwa uwezo wako baba kamua usitumie irizi/ zuga vuruga hali ya hewa au kata gogo/ vurumisha onesha kama una usongo bwana mdogo/ haya vipi?..tena upanga east upanga cost yuupi / karibu basi tule dupu m2 the p anainyaka flag natambaa na chaki/ narusha fataki fi fi fikiri kwanza kabla ya kutenda mwanangu/ naanza namba 2
Hiyo hiyo ndo gia yangu mwanangu leo kitu kinanda mizuka inapanda yanantoka maganda...._
π₯π₯π₯π₯π₯π₯
Cha kwanza mimi kuhusu inshu ya m2the p kumtaja katika lycris ( mashairi) yangu katika wimbo wa "kamua" ni kama ifuatavyo..
Kwanza mimi na M2the p tulikuwa tunakaa nae pamoja kwenye Gheto moja ,..
nilikuwa nakaa sehemu moja panaitwa " sinza " kule kule mtaa wa namaga karibia na studio ya Bongo Records kwa p funk majani...
Tulikuwa Tunaishi nae Gheto moja mimi msanii M2the p na brother soggy doggy...
Kwa hiyo wakati naandika yale mashairi ya hii Ngoma ya ' kamua"
Muda huo nimetoka kwa p funk majani kuchukua ile beat naifanyia Mazoezi Gheto.
Sasa siku hiyo tukiwa wote pamoja mule Gheto mimi Msanii M2The p na brother soggy doggy huku mimi nikiwa naandika zile lycris kwa umakini nikisikiliza ule mdundo wa Beat..
"Yaani!! Mimi , M2the p & soggy doggy tulikuwa Tunaishi pamoja ndani ya Gheto moja na tuna lala kwenye kitanda kimoja mtu tatu (3) . Kitanda cha futi sita kwa sita Enzi hizo..
Nikasema siwezi kumaliza Verse bila hata kumpa shavu hata mshkaji wangu mmoja ..
na mimi nikamuweka jamaa & Rafiki yangu M2the p..
nikampa shavu rafiki yangu Tunaeishi nae Gheto moja..
π₯π₯π₯π₯
Kuanzishwa kwa Crew ya Tmk Enzi..
hizo mimi nakumbuka kulikuwa na hizi Tour moja tulienda kigoma, Arusha na kisha tukamalizia jijini Mwanza..
Na ilikuwa ni kwenye kipindi cha Album ya juma nature inaitwa " Ugali" kama sikosei ..
Sasa wakati Tupo kwenye hiyo Tour
Wasanii wote tulikuwa Asilimia kubwa tulikuwa tunatokea Dar es salaam mtaa mmoja wa Temeke..
Katika hiyo Tour Nlikuwepo mimi kr , chege, yp & dash, juma nature na swebe msanii wa filam ( Bongo movie)
Baada ya kumaliza pale show ya mwisho jijini Mwanza ,..
Itaendelea...