KTDA inashirikiana na Kenya Railways kusafirisha chai kwa SGR

KTDA inashirikiana na Kenya Railways kusafirisha chai kwa SGR

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
Na Tom Wanjala

1642638236384.png

Viwanda vinavyosimamiwa na Wakala wa Maendeleo ya Chai Kenya (KTDA) sasa vitaweza kusafirisha mazao yao kupitia njia ya Reli ya Standard Gauge (SGR) kutoka Nairobi hadi Bandari ya Mombasa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.

Chini ya mpango huo, chai kutoka viwanda vinavyosimamiwa na KTDA itasafirishwa kutoka kaunti zinazolima chai hadi Nairobi Freight Terminal ambapo itapakiwa kwenye mabehewa ya Kenya Railways na baadaye kusafirishwa hadi Bandari ya Mombasa.

Safari ya kwanza kutoka kwa ushirikiano huo ilishuhudia wiki moja lililopita ambapo KTDA ikisafirisha makontena 31 sawa na tani 800 kupitia SGR.

“Tunafurahi kuwa na ushirikiano huu nanyi. Ninawahakikishia kuwa Shirika la Reli la Kenya liko kwenye jukumu hilo. Tuna uwezo wa kutosha kushughulikia mizigo yote ambayo inaweza kusafirishwa kwa njia yetu," Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la reli la Kenya-KRC, Philip Mainga alisema katika taarifa.

Shirika hilo linashirikiana na KTDA kuwasafirishia wakulima chai kutoka Nairobi hadi Mombasa wakati ambapo limenufaika na agizo la sera ya serikali la kusafirisha bidhaa hadi Nairobi na mikoa mingine ya kando kutoka Bandari ya Mombasa kupitia SGR.

Akiongea kwenye hafla ya kusafarisha majani chai kwa mara ya kwanza kwa njia ya SGR, mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli la Kenya Phillip Mainga alihakikishia wadau wa KTDA kwamba kuchagua usafiri wa reli mpya ya kisasa ya SGR, ni chaguo bora zaidi kwa sababu ya manufaa yaliyopoo.

Kando na kuwa majani chai yatakuwa salama, Mainga alidokeza kuwa SGR pia itahakikisha kuwa majani chai yanafika Mombasa kwa wakati unaofaa na kuokoa muda ambao mwingi.

“Tunafurahi kuwa na ushirikiano huu nanyi. Nina wahakikishia kuwa Shirika la Reli la Kenya liko imara kwa kutekeleza majukumu yake. Tuna uwezo wa kutosha kushughulikia mizigo yote. Kwa sasa tunaendesha treni 9 hadi 11 za mizigo kila siku kati ya Mombasa na Nairobi na tunaweza kufanya hata zaidi ikihitajika,” akasema Mainga.

Bw. Mainga aliongeza kuwa ushirikiano huo utapunguza msongamano wa magari barabarani. “Kusafirisha chai kupitia shirika la reli kunamaanisha kuwa barabara hazitakuwa na msongamano kwa sababu treni moja inaweza kusafirisha kiasi ambacho kingechukua malori mengi kusafirisha kwa barabara. Leo tunasafirisha kontena 31 za chai kwenye treni moja. Hii ingechukua malori 31 kwa barabara. Kwa hivyo tunafurahi kuwa katika ushirikiano huu na KTDA kwa sababu Huduma ya Usafirishaji ya Madaraka Express ni chaguo la haraka, salama na linalofaa zaidi,’’ alisema.

Akizungumzia hilo, Mwenyekiti wa KTDA Holdings Limited, Bw. David Ichoho, amesema shirika hilo linafanya majaribio ya kutuma vifurushi 20,000 kwa wiki, huku likiendelea kurahisisha mchakato wa uhamaji kamili kutoka kwa usafiri wa barabara hadi reli.

Ripoti ya Utafiti wa Kiuchumi ya 2021 iliyotolewa na Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS), inasema kiasi cha mizigo iliyosafirishwa kupitia SGR kiliongezeka kwa asilimia 4.8 kutoka tani milioni 4.2 mwaka wa 2019 hadi tani milioni 4.4 mwaka wa 2020.
 
Zao la chai Ni mhimu Sana na mti wa mchai hauzeeki unaweza kudumu zaid ya miaka Mia tangia ulipopandwa. Nimeona mkoa wa njombe wakulima wengi wamehamasika kupanda hili zao. Namm natoa wito kwa serikali kulitazama vizuri hili Kuna makampuni hawalipi mishahara wafanyakaz kwa wakati kwa kisingizio Cha corona
 
Haina sifa ya kuitwa SGR maana imejengwa chini ya kiwango sana alafu inatumia dizeli
 
Back
Top Bottom