Tabby nimefurahishwa na maboresho uliyoyatoa. Ni kweli kwamba ku socialize kazini kuna muda wake. Mfano wakati wa tea break au lunch time. Pia haifai watu ku socialize muda wa kazi. Kusudi langu la kuweka ujumbe huu ni kuwaasa watu kujenga mahusiano mazuri na wafanyakazi wenzao ili waweze kuepuka stress kazini. Ukweli ni kwamba ku socialize kazini kunategemea mind-set ya mtu mwenyewe, kuna wale hupenda kupiga soga muda wote na kuna wale ambao hu socialize muda mwafaka..mfano kabla ya saa mbili asubuhi au muda wa lunch...Chochote chenye manufaa chaweza kuwa na madhara kulingana na matumizi kwa mfano kuna wale wanaotumia WhatsApp kurushiana picha, video clips na message za kingono ngono na mambo ya kipuuzi muda wote( Brain cell killers). Pia kuna wale wanaotumia WhatsApp katika kujuzana habari za kujenga na mambo yenye manufaa. Kwa kifupi ku socialize chanya kuna manufaa kwa mfanyakazi.