KUA UYAONE.
Nilizanini majengo, marefu yalopangana
Nikahisi na viungo, vinono vilivyonona
Hivi nilimeza tango, na ya leo sio jana
Kumbe kua uyaone, fumbo lisilo kikomo.
Nilibuni ni kisomo, misimbo kupata mia
Huko hakuna ukomo, ukweli nikapania
Mbali na vile vipimo, tegua si kutusua
Kumbe kua uyaone, fumbo lisilo kikomo.
Eti kuwa myenyekevu, nikanywa na nikalewa
Mtego ukawekwa wavu, ukaribu kwao chawa
Ona chanzo cha waovu, kuzifunika ngekewa
Kumbe kua uyaone, fumbo lisilo kikomo.
Wabaya walipe mema, simango ni kujikosha
Kipeke peke unyama, Kombaini yaenyesha
Wanyonge kuwapa bima, kipona wasurubisha
Kumbe kua uyaone, fumbo lisilo kikomo.
Anguko na kuinuka, lengo kuu kufundisha
Kolezo kumakinika, dosari kurekebisha
Hizi zote ni pirika, ya dunia kuonesha
kumbe kua uyaone, fumbo lisilo kikomo.
Haya sio hitimisho, mengi muno uibuka
Bila pata suruhisho, ni vingi uharibika
Mbali kuwa kichekesho, na wengine uteseka
kumbe kua uyaone, fumbo lisilo kikomo.
Sina nia kuchachisha, bali ni kuchachusha
Palipo kukasirisha, sindano inaponyesha
Mafupi haya maisha, japo yanaangaisha
kumbe kua uyaone, fumbo lisilo kikomo.
Mauti kama dirisha, wachache uwapumzisha
Yanao wanusurisha, myororo uudumisha
Kihama chanfikirisha, haya ninayotoresha
kumbe kua uyaone, fumbo lisilo kikomo.
Katika kupembua kauli mbalimbali za wasomi na wanafalsafa hasa wa kigiriki na Afrika kuhusu maisha. nimepata kubaini haya kupitia kazi zao.
"Dunia uwanja wa fujo"
Jibu langu : Ni kweli, lakini pia dunia ni uwanja wa mazoezi
Rejea diwani yangu ya sauti ya mwalimu.
"Maisha hayana maana"
Jibu langu : maisha yana maana, tena kubwa sana kulingana na mapokeo au matokeo ya matendo ya mwanadamu yawe mema hama mabaya na uenda siku ya kihama ikatoa jibu sahihi rejea shairi langu "kua uyaone" japo ni fumbo lisilo kikomo". Licha ya wengine kupata furaha hama kuikosa, lakini ni jambo jema kuipata wewe mwenyewe pamoja na kisha kuishiriki kwa wale wanaoikosa.
Kuna "wazanaishi" hoja yao ni kuwa suruhisho la matatizo ya mwanadamu ni kifo.
Jibu langu : hoja hii ni dhaifu sana sababu sisi ni mashahidi wanaoshuhudia migogoro inayotokea baada ya watu wetu wa karibu hata wa mbali wanapokuwa wametutupa mkono, hiwe ni migogoro ya mali au maumivu ya kutozibika kwa mapengo yao, hivyo matatizo uongezeka badala ya kufika kikomo.
"wingi wetu hasa vijana tunabeba hoja hii na kuyaona maisha yetu pamoja na uhai wetu kuwa havina thamani yoyote na kufikia hatua ya kujizawadia vitanzi "kujiua" au kukengeuka baada ya kuikosa "furaha" yaani maisha na kuyasahau mateso tutakayopitia hama yale majonzi tutakayo waachia jamaa zetu". Kumbe kifo si suruhisho la matatizo yamwanadamu. Rejea shairi langu "Kua uyaone" ....mauti kama dirisha, wachache uwapumzisha...
... yanao wanusurisha, myororo uudumisha...
hii ina maana kwamba unaweza kuona kifo ni suruhisho la matatizo "dirisha" lakini wale wanao bakia wanaweza kuendelea kupitia majonzi hivyo kifo sio suruhisho la matatizo ya mwanadamu. Labda kihama ndio kinaweza kutoa suruhisho.
"Tuitafute furaha tena kwa kiasi, kuikosa kusitujaze kakasi" kwani hatujui siku wala saa"
Nini maana ya maisha
Nitajibu kwa kuhusisha mwanadamu na sio jumuhisho la vitu vyote vinavyotokana na kazi ya uumbaji wa Mwenyezi, japo mwanadamu ni sehemu ya kazi ya Mwenyezi katika uumbaji.
Maisha ni utafutaji wa furaha ya moyo katika jamii tunayoishi.
Hivyo kama ningelikuwa mwanazuoni mkubwa hii ingelikua nadharia yangu kuhusu maisha.
maisha ni "furaha"
Nitaulizwa vipi kuhusu majonzi, hasira, wivu, tamaa??
Jibu: vitu hivi ni matokeo ya kukosa maisha yaani furaha. Japo huruka ya mwanadamu katika kukosa kiasi uzalisha "tamaa au wivu" rejea maandishi ya "kuweni watu wa kiasi"
(Adamu na Hawa) walipewa maisha yaani "furaha" lakini tamaa, na hule uongo wa nyoka ukatukosesha furaha" maisha.
Utasikia bado ninatafuta maisha, hii ni sawa na kutafuta furaha.
Nimepigiwa na maisha, hii ni sawa na kusema nimekosa furaha au nimeumizwa kwa kukosa furaha.
TAHAMALI: Kuna tofauti kati ya maisha na uhai/uzima. na uhai ndio unatupa nafasi ya kupata maisha "furaha". hivyo katika maombi yetu tuombe uzima ili kupata furaha "maisha", pale utakapoomba uzima huku ukiwa umebeba furushi la majonzi, mateso na maumivu wapo watu wenye maisha watakuja kushiriki nawe katika maisha.

Upvote
1