Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Makuti ni majani ya minazi yanayopatikana katika mikoa ya kando ya bahari hasa katika nchi za kitropiki. Makuti husukwa viungo na viungo hufungwa kwenye miti au mbao za nyumba ili kuzuia jus na mvua na kujistri.
Makuti hushurubu
joto la jua na kuifanya nyumba kuwa na nyuzi joto ya wastani hata kama nje ni jua kali la kiangazi. Kwa miaka mingi watu wa kipato chachini hata katika mimi mikubwa ya Pwani walitumia makuti katika ujenzi wa nyumba zao.
Ukitaka kuepuka gharama za Air Condition hasa kipindupindu cha kiangazi unaweza kujenga kibanda nyuma ya nyumba na kuezeka paa la makuti. Unaweza kuweka bustani nje au bwawa la kuogelea, ndani ukaweka viti, meza hata TV na fridge ya vinywaji. Sehemu hii ikawa ya kupumzika mchana.
Tatizo kubwa ni uhaba wa viungo na makuti uanojitokea siku hizi. Ni kuwa watu wengi wameacha kilimo cha minazi?