Kuaga Kwa Mwenye Njaa...

Kuaga Kwa Mwenye Njaa...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Nashika tena kalamu, kwa Jina lake Karimu,
Naishika kitalaamu, nashika kiufahamu,
Napanga tungo adhimu, kama gwiji na mwalimu,
Kuaga kwa mwenye njaa, huaga na haondoki!!

Yametokea nyumbani, siku si nyingi jamani,
Hapa kwetu kijijini, nilipokea mgeni,
Mida yenyewe jioni, Mama Chanja yu jikoni,

Karibu bwana Shabani, kwanza u habari gani?
Wazima huko nyumbani, watoto wa hali gani?
Watupa hofu mtani, mbona mida ya jioni?

Wakijiji samahani, napita tu mtani,
Naenda kwa bwana Joni, kile kijiji jirani,
Napita niko mbioni, niwasabahi watani,

Alhamdulillahi Shabani, kutujulia hali mtani,
Twamshukuru Manani, katupa siha mwilini,
Kaepusha tafrani, mwenye enzi wa Mbinguni,
Kuaga kwa mwenye njaa, huaga na haondoki.

Chanja mwambie dada, mgeni amesimama,
Akupatie kigoda, Shabani aje kutama,
Chukua chupa ya soda, nenda kwa bwana Mrema,

Wakijiji samahani, mimi sikai mtani,
Nilivyosema mwanzoni, mwenzio niko mbioni,
Naenda kwa bwana Joni, kabla ya giza jamani,

Soda ntaiongojea, ni sunna naipokea,
Kisha ntaendelea, kule nnakoelekea,
Nisije nikachelea, mwisho nikaja potea,

Jamani vipi jikoni, Mama Chanja kulikoni?
Ana haraka mgeni, kasema yuko mbioni,
Leteni vitu mezani, vya kuku na biriyani,

Niwie radhi mtani, soda yatosha jamani,
Namuwahi bwana Joni, siku nyingine mezani,
Ila hilo biriyani, ni sunna nayo mtani!!
Kuaga kwa mwenye njaa, huaga na haondoki!

Dakika 45 baadaye...

Nawashukuru watani, tamu hili biriyani,
Sasa ni giza njiani, wacha nirudi nyumbani,
Kwenda kwake bwana Joni, siku nyingine mtani,

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Dah! Kwahiyo Kesho tunafinya Biriani la bwana John
 
Back
Top Bottom