Wakuu nipende kuwasalimia kwanza,
As-salamu alaykum. Bwana Yesu asifiwe.
Kama kichwa kinavyosema hapo juu, mimi ni mtu ninayefuatilia kwa kiasi mambo ya mitandao lakini kufuatilia hakumanishi najua mambo yote.
Leo nimeona nije kuomba msaada kwa anayejua jinsi ya kuagiza bidhaa mtandaoni, namaanisha katika maduka ya mtandaoni kama Amazon, eBay, Ali Express n.k.
Naomba kufahamishwa ni mambo gani yanatakiwa au nifanye nini mpaka hatua ya kupata bidhaa nitakayoiona katika duka la mtandao husika.
Natanguliza shukrani, Asante.