Kuagiza Toyota Raum kutoka Japan mpaka inaingia barabarani itagharimu kiasi gani?

Msaada kwa wale wataalamu
Kuagiza Toyota Raum kutoka Japan mpaka inaingia barabara itagharimu kiasi gani?
Chukulia hii pichani ya mwaka 2006

#1. Kuifikisha DAR ES SALAAM + Clearing = US $2,540 x 2,300TZS [ Rate halisi kwa TZS utaikuta benki wakati wa kufanya deposit] = TZS. 5,842,000

#2. Makadirio ya gharama za TRA kwa kutumia hii link: Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System
Tunapata TZS. 5,220,548.70
Jumla: 11,062,548.7

NB
: Hapo kuwa na ziada kama laki 5, gari inaingia barabarani

Karibu: www.bit.ly/101buy4me
 
SBT wako vizuri zaidi. Nafasi yao ya kujadiliana bei kwa WhatsApp, baruapepe na kwa kuongea ni kubwa na iko wazi sana.
Wajaribu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa msaada wa wengine wanaotaka kujua haya mambo.

Bei za gari hazifanani hata kama ni aina moja. Kuna vitu vya kuzingatia vinavyofanya bei iwe juu au chini.
Mfano:
1. Mwaka wa kutengenezwa gari.
2. Km ilizotembea japo hii sio kigezo sana.
3. Kampuni unayoagiza magari, hapa zinayofautiana kutokana na ubora wa magari yao na namna wanavyosafirisha hayo magari kutoka japani hadi kwa mteja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…