Kuahirishwa kwa mechi ya watani wa jadi, huwa namwelewa sana king msukuma

Kuahirishwa kwa mechi ya watani wa jadi, huwa namwelewa sana king msukuma

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Wazo la kuahirishwa kwa mechi bila shaka limetolewa na msomi wa chuo kikuu aloyeaminiwa kupewa kazi kwa usomi wake.Huyu hakuangalia maslahi ya washabiki amabao tangu saa moja asubuhi wameingia uwanjani.

Kama vile haitoshi,makosa yameshafanyika,kulikuwa bado na nafasi ya kupunguza maumivu,msomi mwingine kutoka club ya mpira,akaamua kuchagua matumizi ya kanuni badala ya busara.Bila kufikiri anayeumia si TFF,wala serikali,bali mashabiki ,na wengine wametoka mbali sana,akaamua kuonesha usomi wake kwa kusimamia kanuni.

Natamani hiyo kanuni isomwe kwa lugha ya kisheria.
Kuahirisha mechi ni sawa na kusogeza muda wa mechi mbele?
Kama kuahirisha mechi ni sawa na kusogeza mechi mbele, basi ninazidi kuamini wasomi wetu waliohusika kutengeneza hizi kanuni,wana haki ya kupokea hoja zote za mbunge wa Geita mh.Musukuma.

Tumeambiwa kuwa yalikuwa maelekezo ya wizara.Hao watu wa wizara wanasubiri nini kutoa taarifa.Au ndio mpaka jumatatu waingie ofisini?

Hizi elimu za kitanzania mbona huwa zipo kumkandamiza tu mtu mnyonge?
 
Wasomi wengi nchini hawajui maana ya elimu. Ndiyo hawajui! wao wanafanya mambo kama maroboti na ndiyo maana mpaka leo SAMIA anatumia maneno ya dharau kama vile VIJITV VYA MKONONI, VIUJAMBAZI. yaani ni aibu.
 
Msukuma akiongea anashambuliwa kisa darasa la saba, kina dalali pamoja na mambo makubwa waliyofanya wamezuiwa kugombea TFF kisa hawana elimu inayostahili sasa visomi uchwara ndio vinaharibu kila kitu yaani wanashirikiana na utopolo kuharibu mechi
 
Back
Top Bottom