marandu2010
JF-Expert Member
- Aug 7, 2010
- 1,201
- 446
Kujiajiri ni kuzuri kuliko kuajiriwa kama umejiandaa kikamilifu kwa maana kwanza uwe umeajiriwa, ukajikusanyia uzoefu pamoja na mtaji hapo unaweza kufanya kitu.
Hata hivyo bado unatakiwa angalau uwe na akiba ya kukutosha kuishi miaka si chini ya miwili bila kutegemea biashara yako. Mimi niliacha kuajiriwa nikiwa na Mshahara was Shs. 1,500,000 nikaanza biashara yangu (Ya kitaalam siyo Buy and Sell), kwa mwaka wa kwaza, biashara hii iliweza kunilipa Shs, 200,000 tuu kwa mwezi baada ya kodi, mishahara na gharama nyinginezo. Kwa mwenye moyo mwepesi si raisi uache 1,500,000 ukaumize kichwa kwa TShs 200,000. Leo hii ni tofauti kidogo, ofisi imeajiri graduate watano (full time), Part time wawili lakini baada ya kusota miaka mitatu
Niliwahi kusoma kitabu kimoja cha mambo ya ujasiriamali ameandika mfilipino mmoja (sikikukmbuki title, nitajaribu kukitafuta nishee) anasema kama umeajiriwa si vema kuacha kazi kwenda kujiajiri. Unatakiwa ujiajiri wakati unaendelea na kazi mpaka huo mradi wako utakapoweza kukupatia mara mbili ya mshahara wako ndo uache kazi ukasimamie mwenyewe mradi wako ili kuongeza kipato zaidi.Kujiajiri ni kuzuri kuliko kuajiriwa kama umejiandaa kikamilifu kwa maana kwanza uwe umeajiriwa, ukajikusanyia uzoefu pamoja na mtaji hapo unaweza kufanya kitu.
Hata hivyo bado unatakiwa angalau uwe na akiba ya kukutosha kuishi miaka si chini ya miwili bila kutegemea biashara yako. Mimi niliacha kuajiriwa nikiwa na Mshahara was Shs. 1,500,000 nikaanza biashara yangu (Ya kitaalam siyo Buy and Sell), kwa mwaka wa kwaza, biashara hii iliweza kunilipa Shs, 200,000 tuu kwa mwezi baada ya kodi, mishahara na gharama nyinginezo. Kwa mwenye moyo mwepesi si raisi uache 1,500,000 ukaumize kichwa kwa TShs 200,000. Leo hii ni tofauti kidogo, ofisi imeajiri graduate watano (full time), Part time wawili lakini baada ya kusota miaka mitatu
hilo pia neno, fikiria mimi ni msomi,unanishauri nikimbilie wapi kati ya haya mawili???? na ikiwa nitachagua A au B,nifanye vipi ili nifanikiwe zaidi???ubunifu mdogo sana Tanzania,wafanyabiashara wengi sio wasomi na wasomi wengi hawapendi kufanya biashara.
Jiulize serikali inafanya nini kuimprove bizness startup enviroment!