Kuajiriwa ama kujiajiri

Mku inabid ubukue vizuri hiyo book ili utupe nassi mawili matatu
 
Wakuu nime jitahidi kusearch hadi nimekutana na hili somo,very nice.kweli JF ni kiboko.
 


Mkuu umenivukisha mahali maana naona kama napita kwenye hali kama ya kwako. Nilipotoka tu chuo nilichukia mno kuajiriwa. Ila nilijipa muda wa miaka minne tu wa kuandaa na kuendeleza biashara yangu. Miaka minne ilipoanza kukaribia kuisha mwaka jana 2011, nilikuwa bado sijaweza kuifikisha biashara yangu nilipokuwa nimeplan iwe. Kwa kuwa nilisha panga kuacha nikasema sitarudi nyuma lazima ni-terminate contract. So, mwaka jana nimeacha kazi, miezi miwili iliyopita ilikuwa migumu sana kwangu, ila naona hali ya ofisi yangu inaanza kuonyesha matunda mazuri.

Kabla ya kuacha kazi niliwashirikisha watu plan yangu, zaidi ya asilimia 90 hawakunielewa, ndipo nilipoamua kuchukua uamuzi binafsi, hata ndugu sikuwaambia kama nimeacha kazi maana lazima wangelikataa wazo langu.

Ninachoweza kushauri,kama upo kwenye ajira,
1. Fahamu nini unachotaka kufanya pindi utakapo kuwa nje ya ajira,
2. Anza kuweka mkakati wa kukifanyia kazi ukiwa ndani ya ajira.
3. Weka muda pia kwamba unataka kuajiriwa mpaka lini, let say, mwaka 1, 2 au 3..n.k, bila ku-set muda utajikuta una mawazo ya kujiajiri lakini lini hujui na utaendelea kubakia kwenye ajira maisha yako yote ukiwa na wazo la kujiajiri mwenyewe. Pia uwe strict katika muda ulio set, na hapa ndipo maamuzi magumu yanapojitokeza unapotaka kuendena na plan yako.
4. Tafuta ushauri kwa watu tofauti walioko kwenye biashara na haswa biashara unayotaka kufanya na ujifunze kutoka kwao..

All the best.
 
Bora kufanya yote mawili na ndivyo wengi wanafanya.
 

wakuu tatizo la uoga wa watanzania kutake risk linachangiwa na na vitu viwili.
1.mfumo wa maisha tuliyolelewa-tangu tukiwa wadogo tunaambiwa soma uje kupata kazi nzuri,na sio soma uje kutengeneza ajira.sasa hii inatujenga hadi tunapomaliza chuo kuamini kazi nzuri ni ile tu unayoenda kuajiriwa na si vinginevyo.na hata hivi leo mtu akionekana asbuhi hajavaa shati na na tai na nakachomekea anaonekana hana future nzuri au shuguli maalumu
2.mfumo wa elimu,elimu yetu inatuandaa kukariri na kufaulu mitihani tu na sio kutufikirisha kutatua matatizo.pia kujiajiri kunahitaji kujituma na kufanya kazi kwa bidii amabalo hilo wataanzania wengi hawako tayari kwasababu kwenye ajira watu uwa mda wote wana feel proud kuwa na kazi lakini si utkelezaji wa majukumu kwa ufanisi.
Nb:kujiajiri kwa mazingira ya sasa ya ajira ni best option,maslahi ni kidog sana kwenye ajira.ni raha sana asubuhi unaamka unaelekea ofisini kwako.
 
Bora kufanya yote mawili na ndivyo wengi wanafanya.

Nakuelewa sana Husninyo ni kweli wengi wanafanya hivi na ndio sababu wengi wanashindwa ku-take off.Lazima kuchagua moja hapa na kuwa tayari ku-take risk ili kufikia malengo husika hakuna kitu kama kufanya vyote kwa pamoja(isipokuwa kwenye zile hatua za awali kabisa za kujiajiri) kwa sababu lazima kuna kimoja kitazorota au unaweza kuvipoteza vyote.
Ajira inahitaji kuwekeza umakini ma muda wa kutosha na kujiajiri kupo hivyohivyo.
 
Bora ujiajiri hata kwa kuuza sigara unatoka kimaisha kuliko kusubiri ajira ya mwisho mwezi
 

nimekusoma ila kujiajiri na kuajiriwa vyote vina faida na hasara zake. Naona humu imekuwa fashion kila anaekuja anasema bora kujiajiri wakati wao wenyewe ni waajiriwa hadi wanazeekea kazini. Mambo kama haya ni vizuri kumwelesha mtu kwa pande zote mbili.
 
We Husnino ukimaliza phD jiajiri hata kufuga kuku ni shwari tu imradi una ofc yako
 

Hii ni nzuri cuz unaweza ukayumba wakati biz ipo mwanzoni na ajira ikakusaidia kuisukuma.
 

umesema sawa mkuu,lakini hebu angalia serikali imeweka mikakat gani kumsaidia kijana huyu ambaye ana nia ya dhati kabisa ya kujiajiri?kwa sababu hana mtaji,kazi hana,na ana mahitaji ya kila siku yanamkabili,afanye nn? Au nini kifanyike? Asante mkuu kwa mchango.
 
mkuu thats what life is all about; HAPPINESS, ABUNDANCY, SERVING OTHERS, FREEDOM, LIFE STYLE OF YOUR DREAM........

TRAVELLING THE WORLD IMETULIA SANA.

hivi pesa za retirement hz hz za madafu zinaweza zikatupa hivyo vitu kweli? Na ukumbuke dependence ya wandugu with your amount fixed,hebu nijibu mkuu,otherwise thanks
 

Kwa hiyo mkuu unataka kuniambia ile elimu ya ujasiriamali tuiite biashara? Mm ninaweza kusema kwa upeo wangu wa wastani kuwa kila kitu kinakwenda kwa elimu,without education the mission is blank,isipokuwa elimu haipatikani darasani tu,hata kitaa waweza pata elimu,au unasemaje bwana mkubwa? Thanks for your contribution
 
kuna fursa nyingi sana katika kujiajiri. ni wewe tu kuwa na moyo wa kijasiriamali na kujua wapi utapata mitaji ya kujiendesha, na mikakati ya kuendeleza biashara yako

Ni kweli mkuu,spirit ya entrepreneurship ni muhimu sana,hii itakusaidia kupenya pindi utanda wa changamoto utakapotokea.
 
Wakuu nime jitahidi kusearch hadi nimekutana na hili somo,very nice.kweli JF ni kiboko.

mkuu,hapa ndio mahali pake,ila usichukue haya materials kwa ajili ya kujibu mtihani,yachukue kwa ajili ya practical application ili ujikuomboe kiuchumi na uinjoy matunda kama freedom nk,shukrani mkuu.
 

Mkuu nilisahau kukupongeza kwa kuweka neno "ukiweza" bilashaka lina maana sana hapo.
 

Nashukuru mkuu kwa mchango mzuri,kikubwa ni kuyaweka katika matendn ili tuweze kufanikiwa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…