kuandika jina ubavuni mwa gari lako: hii sheria ina umuhimu gani leo?

kuandika jina ubavuni mwa gari lako: hii sheria ina umuhimu gani leo?

Ntumami

Senior Member
Joined
Sep 3, 2010
Posts
127
Reaction score
23
habari wana JF

Leo ningependa kulifikisha hili kwenu tulitazame sote kwa pamoja, huwa ninaona magari yameandikwa majina ya wamiliki ubavuni, mara nyingi kwa saloon ni karibu na milango ya mbele. Leo mtu mmoja akaniambia yeye alikutana nayo hiyo alipoenda kulipia faini mojawapo polisi akaambiwa hata kutokuweka jina ubavuni pia ni kosa na unaweza lipa faini!! sasa swali langu ni kuwa kuna umuhimu gani wa leo hiii kwa sheria hii kuendelea kufanya kazi?

sioni umuhimu wa kuandika jina langu kwenye gari langu!! ila nabanwa na sheria!!!

kama kuna polisi/lawyer naomba aseme neno ama afikishe hili huko juu
 
Kwa gari la biashara au la mizigo hiyo ni lazima na kosa kisheria. Magari ya binafsi siyo lazima.
 
Kwa gari la biashara au la mizigo hiyo ni lazima na kosa kisheria. Magari ya binafsi siyo lazima.

Kama magari binafsi siyo lazima mbona polic wanasumbua kama haunayo? Hasa ukisafiri kwa magari binafsi kwenda mikoani huwa wanakuwa wasumbufu sana na kuishia kudai chochote kitu.
 
Kama magari binafsi siyo lazima mbona polic wanasumbua kama haunayo? Hasa ukisafiri kwa magari binafsi kwenda mikoani huwa wanakuwa wasumbufu sana na kuishia kudai chochote kitu.

Angalia kifungu cha kumiliki magari kama pick up, double cabin, hiace za familia au kosta za mafamilia.
 
Sipati picha. Gari langu liandikwe Oswald Muluzi, P. O. Box 0. Blantyre. Malawi!
 
Kwa anaijua hiyo sheria naomba atuwekee hicho kifungu hapa
 
CC: Mliopo jeshi la polisi , wanasheria wa serikali na wanasheria wanaoijua sheria hii
 
Back
Top Bottom