mohammed Arafatt
Member
- Jul 28, 2022
- 7
- 4
Ni katika hoteli moja ya kifahari katika jiji ambapo wapenzi wawili waliopendana sana walikuwa wakivinjari maisha yao kwa kuponda raha kedekede zilizoakisi uwezo wao wa kifedha uliotokana na mishahara minono waliyoipokea mwisho wa mwezi.
Wapenzi hao wawili ambapo mmoja alikuwa ni daktari na mwengine akiwa ni mwanajeshi hodari katika taifa, waliishi pamoja kwa muda usiopungua miaka mitano huku matarajio ya kila mmoja wao yakiwa ni kuja kufunga ndoa na mwenzio wake hapo baadae.
Katika usiku mmoja wa furaha, mwanadada aliyejulikana kwa jina la Irene, daktari bingwa wa magonjwa ya akiba mama na watoto aliibua mada nyeti kuhusu swala la mahusiano yake yeye pamoja na mpenzi wake Donatus akimtaka mpenzi wake huyo kuanza kufikiria swala la kujitambulisha nyumbani kwao ili waweze pata radhi za wazazi na ikibidi wafunge ndoa.
"kipenzi, ni miaka mingi sana imepita toka tuingie kwenye mahusiano hivi unanipenda kweli?".
Aliuliza Irene ambaye kwa muda huo alikuwa amelala juu ya kifua cha mpenzi wake Donatus. "ooh yes babe, kwani huamini katika hilo?".Aliuliza Donatus huku akichezea chezea nywele ndefu za Irene ."Naamin kipenzi ila sijajua ni lini utanifany niwe wako wa maisha".
Alisema Irene kwa sauti ya kudeka.
"Tunaenda kesho mpenzi".
"What!". Alisema Irene kwa sauti ya mshtuko baada ya kusikia kauli ile kutoka kwa mpenzi wake Donatus. "Ndiyo kipenzi, hata mimi nataka sana uwe wangu wa maisha .so, by suprize kesho asubuhi tutaanza safari ya kwenda kijijini kwa wazazi wako kujitambulisha".
" thank you so much kipenzi.". Alisema Irene kwa furaha huku akimkumbatia mpenzi wake. siku mbili baada ya safari ya kuelekea kijijini kwa wazazi wa Irene kutimia, familia ya bwana na bibi Ezekiel ikaitisha kikao cha familia kilichohudhuriwa na wazazi wa Irene, pamoja na kaka yake huku yeye pamoja na Donatus wakiwa ndio ajenda kuu katika kikao hicho." kijana unaishi wapi?".Aliuliza mzee Ezekiel."
Aaah..mzee mimi naishi Arusha , maeneo ya Ngarenaro Ndiyo sehemu ambayo huwa naishi nikitoka kambini ".
" kwahiyo wewe ni mwanajeshi si Ndiyo?".
" Ndiyo mzee".
" Anhaa na vipi unaweza kutupatia historia fupi kuhusu wazazi wako asili yenu na kila kitu".
" aaaa...familia yangu mimi inapatikana Dodoma, maeneo ya binge.Ni familia ya beans Albert Mumba ".Alisema Donatus kauli ambayo ilimshtua sana mzee Ezekiel hata akatazamana na mkewe kisha kwa unyonge kidogo akamtuma mwanawe wa kiume ili aende kumletea album chumbani kwake.Ilipoletwa, Mzee Ezekiel akatoa picha moja ya kifamilia na kumpatia Donatus ambapo kwa mshtuko mkubwa Donatus alimuona baba yake katika picha aliyopewa na bwanaa Ezekiel.
Donatus akashangaa na kuuliza ni kwa vipi bwana Ezekiel alijuana na Mzee Albert .Ndipo bwana Ezekiel akaweka wazi kwamba bwana Albert ni kaka yake waliye changia mama lakini walitengana kwa muda mrefu sababu ya ugomvi uliosababishwa na kugombea mali.
Baada ya taarifa hizo za fedheha kutokea Donatus akafanya maamuzi ya kurudi mjini. Baada ya miezi michache kupita zikasambaa taarifa kwamba Donatus ameoa na mkewe tayari ni mjamzito.
Habari hizi zilithibitishwa na Irene mwenyewe baada ya mpenzi wake huyo kwenda kuhudumiwa na aliyekuwa mkewe katika hospitali aliyohamishiwa Irene kikazi.Kwa kujikaza Irene akamhudumia mke wa aliyekuwa mpenzi wake kisha akaomba aweze kuongea na mpenzi wake huyo japo kwa uchache .
Shauku kubwa ya Irene ilikuwa ni kujua ni kwa vipi Donatus ameweza kuoa tena mwanamke mwengine tena mwenye ujauzito wa miezi sita hiyo ndio kusema kwamba Donatus amekuwa akimsaliti kwa kipindi chote walichokuwa kwenye mahusiano.
Majibu mafupi ya Donatus yalimkata mainu Irene baada ya kuomuomba Irene aache kumfuatilia kwani walishaambiwa kuwa wao ni dada na kaka.Jambo hilo lilimuumiza zaidi Irene na baada ya kupata majibu hayo makali hali yake ikabadilika na baada ya siku kadhaa kupita aliamua kuacha kazi na kurudi kijijini kwa wazazi wake.
Hakuwa mtu wa kujichanganya na watu, wala hakutaka kuulizwa sababu za yeye kuamua kuacha kazi.Tabia na mwenendo wa Irene ukabadika kabisa kwani akageuka kuwa mtu wa hasira za haraka muda wote na mara zote alikuwa akijiongelesha mwenyewe.
Wazazi wa Irene walibaki kuilaumu jamii wakidhani kwamba binti yao alirogwa ili asiweze kuendelea na kazi yake ambayo iliisaidia familia yake kiuchumi.Walimaliza waganga wa kienyeji kumtibu lakini haikusaidia kitu na baada ya siku kadhaa Irene hakuweza kuongea tena.Siku moja Irene akakutwa amedondoka chini baada ya jaribio la kutaka kujinyonga kufeli akiwa chumbani kwake.
Akiwa hana fahamu kaka pamoja na wazazi wake wakamchukua na kumpeleka hospitali kwani hali yake haikuwa nzuri kimwili na kiakil.
baada ya kumpeleka hospitali wakaelezea namna ambavyo Irene amekuwa akionyesha mabadiliko ya kitabia na mwenendo.kisha vipimo vikaonyesha kwamba Irene alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa sonona.
Hili lilithibitishwa na daktari baada ya dalili na vipimo kuonyesha kuwa ni kweli kuwa Irene amepata tatizo hilo.
" daktari,vipi binti yetu ataweza kweli kurudi katika hali yake ya kawaida?". Aliuliza mama wa Irene huku machozi yakimlenga.
" bila shaka, tatizo la bint yenu linatibika kabisa na hapa sisi kama madaktari tuna njia mbili za tiba moja ni kwa njia ya mazungumzo baina ya madaktari na mgonjwa yaani mazungumzo tiba, na njia nyingine ni njia ya vidonge ambapo njia hii ni kwa wale ambao wenye dalili mbaya zaidi na pia tunashauri familia kujaribu kutunza amani kwenye familia zao ili kuepusha matatizo yenye kuleta athari katika mfumo wa akili".
Baada ya maelezo hayo, Irene alapatiwa matibabu na baada ya kipindi kadhaa kupita Irene aliweza kurudi kazini na kuendelea na maisha yake ya kawaida akiwa mbali kabisa na matarajio ya kumrejea Donatus kwani akaweza kuukubali ukweli mchungu kwa moyo safi.
Funzo: Jamii inapaswa kutilia maanani swala la afya ya akili kwani tatizo hili limekuwa likiwasumbua watu wengi pasi na wao kujigundua na hivyo kusababisha matukio ya kikatili kuongezeka katika jimii zetu
serikali pia itoe elimu kwa jamii kwa kina ili kuweza kupunguza matokeo mabaya ya tatizo hili kwa watu wa jinsia na rika zote.

Upvote
0