Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kwenye huo mkasa wa kuanguka kwa ghorofa Kariakoo kuna mengi yanasemwa ila linalozungumzwa zaidi ni hili la ghorofa kuchimbwa katika msingi kujenga underground.
Kama ni kweli watu walikuwa wanachimba hilo ghorofa kwenda chini ila kutengeneza huo upuuzi unaitwa underground/basement halafu wapangaji na mawinga wanaendelea kufanya biashara kwa juu kama kawaida basi hakuna tofauti sana na ajali za mabasi yanayosababishwa na dereva wanaoendesha vibaya huku abiria wanamuangalia, kumchekea au kumnyamazia tu.
Nakumbuka Tibaijuka kuna wakati alikuwa analalamikia kituo cha mafuta kilichokuwa kinajengwa barabara kiholela mtaani kwake baadhi ya raia wakawa wanamuona mnoko na mwenye wivu. Kuridhika au kutoguswa na upuuzi unaohatarisha maisha yako ni kushiriki kujimaliza mwenyewe.