Kuanguka kwa Nidhamu na Maadili Kutasababisha Kuanguka kwa Taifa!

Kuanguka kwa Nidhamu na Maadili Kutasababisha Kuanguka kwa Taifa!

HKigwangalla

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2008
Posts
722
Reaction score
971
Leo nimependa kuchangia kidogo tu kuhusu nidhamu na umuhimu wake katika kuleta maendeleo ya Taifa lolote lile, ama ya taasisi yoyote ile, ama ya mtu yeyote yule.

Nidhamu ninayoiongelea hapa ni ile inayohusiana na kuheshimu misingi yote ya maadili, misingi ya kazi na ya maisha; kuheshimu kanuni na sheria zilizowekwa na kufuata maelekezo yaliyopo. Kufanya hivyo kunasadikiwa kuwa ni njia ya kistaarabu. Ni njia ambayo watu waliostaarabika wanaifuata ili kujiletea maendeleo na ili kuishi kwa amani na watu wengine, na mazingira yanayowazunguka.

Maadili ni msingi mkubwa sana wa kuleta maendeleo ya watu. Maadili ni dhana inayowataka watu kuheshimu misingi ya sheria, kanuni na taratibu ili kuweza kuishi kwa amani na usawa na baioanuwai nyingine.

Maadili ni kujua kipi sahihi na kipi si sahihi. Hivyo kuwa na maadili ni kuhakikisha unafanya kila kitu kwa kufuata misingi ya kutazama uhalisia wa uhalali wa mambo kiusahihi wake. Usahihi unachimbua msingi wake kwenye fikra kwamba haya ni yale mambo ambayo watu wengi wenye akili timamu na bila kulazimishwa wamekubaliana kwa pamoja kwamba hili litakuwa hivi, na lile litakuwa vile na hivyo kulifanya liwe ada.

Misingi hii mikubwa miwili isipoangaliwa na kulindwa inaweza kupelekea Taifa kuchelewa kuendelea mbele ama kuanguka tu. Kwa sababu bila kuwa na nidhamu na maadili watu watajifanyia mambo wanayoona wao yanafaa hata kama hayakubaliwi na watu wengi wenye akili timamu. Kwa mfano leo hii tuna tatizo la rushwa, jambo ambalo halaikubaliki kwenye jamii yoyote ile ya wastaarabu – hii ikikithiri tu inatuvuruga sana, tunaona leo hii rushwa kubwa ilivyosaidia kuwapa ajenda wapinzani wa Chama Cha Mapinduzi, jambo ambalo limepelekea kuondoa imani ya wananchi dhidi ya watawala.

Imani ya wananchi inavyozidi kupungua dhidi ya watawala inasababisha migomo na maandamano na hata uasi kwenye baadhi ya nchi – mambo ambayo yanadumaza maendeleo ya Taifa na mahala pengine yameweza kuangusha dola. Ni mtu asiye na maadili tu anayeweza kuchukua rushwa na kuminya haki ya wengine. Mfano mamilioni ya pesa yaliyopotea kutokana na rushwa kusababisha mikataba ya hovyo ya madini kusainiwa yamesababisha serikali kukosa kodi ambayo ingetusaidia kukuza uchumi wetu kwa kujenga miundombinu na pia kuboresha huduma za jamii.
 
Haya mambo badala ya kuishia kuyaweka hapa jamvini tu kwanini huyapeleki kwenye vikao vya juu vya CCM maana huko maadili kuanzia Mwenyekiti hadi tarishi ni ya kusikitisha sana.

Kumbuka ikatolewa kauli ya kulivua gamba ili kukisafisha chama kurudi katika maadili yake ya miaka ya nyuma lakini hadi kesho kutwa gamba halijavuka na maadili ndani ya CCM yanazidi kuporomoka na nchi kwenda alijojo.
 
Ndg BAK, mimi ni mchangiaji mkubwa sana kwenye mambo ya uwajibikaji, wajibu wetu kwa Taifa, uzalendo, uwajibikaji, utu, nidhamu na maadili...na ninatoa mchango wangu kwenye mambo haya si kwa sababu nyingine zaidi ya mapenzi ya dhati kwa nchi yangu.

Nafasi niliyonayo kwa sasa ni ya kusema na kushauri tu, na ninajitahidi kutoa ushauri wangu, kwa viongozi wenzangu wakubwa kwa wadogo na kwa wananchi wenzangu ili tusonge mbele - sababu naamini haya si ya viongozi tu na matatizo yetu kama nchi hayasababishwi na kumomonyoka kwa maadili kwa viongozi tu, bali ni janga la kitaifa, linatugusa sote kwa pamoja...na hivyo ujumbe unapaswa utufikie sote...na tuuelewe na kuufanyia kazi
 
Mkuu HKigwangalla,

Nakubaliana nawe katika yote uliyoyaandika. Tatizo letu kubwa kama nchi ni mmonyoko wa maadili kwa Viongozi wengi ndani ya CCM na hili linachangia sana katika nchi kubaki nyuma kimaendeleo katika kila Nyanja. Nchi kama Rwanda ambayo haina utajiri mkubwa kama nchi yetu na ambayo Wananchi wake waliuana miaka karibu 20 iliyopita katika vita vya wenyewe kwa wenyewe (Watusi na Wahutu) katika kipindi hiki cha miaka 20 wamepiga hatua kubwa sana kimaendeleo na Wananchi walio wengi wenyewe wanaona tofauti ya hali zao za kimaisha ambazo kiwango chake kimepanda kwa kasi kubwa. Sisi katika kipindi hicho hicho cha miaka 20 nchi yetu imerudi nyuma kimaendeleo. Watanzania wengi wanaishi katika maisha yenye ufukara wa kutisha.

Vipato vya wafanyakazi walio wengi wakiwemo Walimu, Madaktari, manesi n.k. vinaongezeka katika kiwango kidogo sana (ukilinganisha na vipato vya waheshimiwa Wabunge na Mawaziri )ambacho hakikidhi kabisa uongezekaji wa gharama za maisha. Matokeo yake kunakuwa na gap kubwa sana kati ya walionacho na wasionacho.

Tumeona huo mmomonyoko wa maadili kutumika na wagombea uongozi mbali mbali nchini kutumia mabilioni ya pesa ili kununua kura kwa kuwahonga wapiga kura. Pia mmomonyoko huo umeleta ufisadi wa kutisha (kama vile wa rada, EPA, meremeta, Kagoda, Richmond/Dowans, mikataba ya madini n.k.) nchini ambayo Watanzania wengi tunaona haina maslahi na nchi yetu. Cha kushangaza wahusika wote wa ufisadi hakuna anayewagusa miaka nenda miaka rudi. Juzi tumemsikia Hosea wa TAKUKURU akilalamika kwamba Serikali imemfunga mikono katika utendaji wa kazi zake.

Miaka ya karibuni tumeanza kuona vipigo dhidi ya Watanzania wasio na hatia yoyote na baadhi kusababisha vifo na sasa tunaanza kulipuana mabomu wenyewe kwa wenyewe!! Kitu ambacho kinasikitisha sana. Haya yote Mkuu yanastahili kukemewa kwa nguvu zote. Na kwa kuwa mwenzetu umebahatika kuwemo mjengoni na labda katika kamati mbali mbali za CCM ukikemea haya kwa nguvu zote sauti yako itasikika na Watanzania tulio wengi tutaiunga mkono bila kujali itikadi zetu za kisiasa.
 
Doc. Hamis;

Wholeheartedly, I agree with you on this issue, and I believe that everybody knows that we have a problem. However, knowing a problem and finding its solution are two different things. For many years, in vain we have tried to address national problems by enacting new laws, forming investigative committees, or conducting lip service campaigns. These approaches haven't worked when Nyerere, Mwinyi and Mkapa were in power. They aren't effective currently and it's time be honest with ourselves and change the course.

Moral and ethical problems are widespread issue in Tanzania. We can blame the leaders at the top because doing that is the easiest thing to do. We blame leaders for everything, but we have forgotten that leaders mirror our characters. They are reflection of what we are as a nation. So if we want to our problems, we have to find a way to solve them collectively, from the bottom to the top and vice versa.

First, we should reform education institutions so they could nurture our people the values of ethics and good characters. So far our students are very busy acquiring knowledge which will enable them to pass their final exams. They will do anything, even applying illegal means, to pass their exams. What do you expect from them when they grow up?

The other thing we can do collectively are the accumulation of national wealth and its distribution. Nations that depend on extraction of natural resources and donation from outside sources for their survival are always riddled with corruption and moral issues. This is exactly the case of Tanzania. For many years, our government is the sole problem solver. However, the way it solves the problems isn't transparent.

If we take efforts to be an open society and transparent, we will excel in many areas without tough laws or TAKUKURU. For example, if Tanzanians know that a percentage of sales taxes is used to build schools, roads and hospitals, they will be proactive and also make their leader accountable. If our election system is fair and transparent, we will elect leader that bring results.

To me your moral and ethical issues facing our country are systematic problems. We have system that is broken.
 
Yakhe HKigwangallah ni aje!? Mbona umeususa uzi wako!? Hii tabia ya kuanzisha threads halafu unapotea si vizuri Mkuu au umetingwa na shughuli za chama na sirikali!?
HKigwa was supposed to "repent" for any wrong doing he had ever committed before posting this stuff here.
 
Dr Kigwangallah,

Ulilosema ni kweli kabisa, maadili ni jambo la muhimu kabisa katika tifa lolote. Mimi niliwahi kuishi marekani kwa muda mrefu sana na nikaona jinsi rais anavyoweza kuwajibishwa na bunge anapokiuka maadaili ya madaraka yake, wabunge (congressmen, congresswomen, na senators) wengi sana waliwahi kufungwa kwa kukiuka madaraka yao, na hata matajiri wengi sana (k.m. Martha Stewart) pia walifungwa kwa kukiuka maadili.

Mimi niliyezaliwa miaka ya hamsini na kupata bahati ya kuishi miaka ya sitini, sabini, themanini, tisini na elfu mbili nina uhakika kuwa mara tu baada ya mwaka 1990 maadili yalianza kuporomoka pole pole katika nchi yetu, na kuanguka kabisa mwaka 2000. Ndiyo maana wabunge kama nyie leo hii mnaweza kufanya lolote bila kuguswa na sheria. Mara kadhaa tumezungumzia Azimio la Arusha, lakini watu wenye akili finyu wamekuwa wakija na mtazamo mfupi wa Azimio hilo la wakati wa cold war. Mzee Mwiny aliyevunja azimio lile huko Zanzibar kwa kutokuona mbali aliwahi kuruka kuwa hawakuvunja azimio hilo bali walikuwa wakiliimarisha wakati ukweli ni wazi kuwa hapo ndipo maadili yalipoanza kuporomoka.

Tulipofikia, tunahitaji mabadiliko ya nguvu sana, siyo tu ya kubadilisha mwenyekiti wa CCM. Na iwapo tutendelea katika njia tuliyo nayo, nina wasiwasi tutaishia kuwa banana republic ambamo kila mtu anachumia tumbo la leo tu kabla halijaoza kesho, siyo kwa vizazi vijavyo.

Kwa sasa hivi CCM ndiyo janga kubwa sana kwa taifa hili leo, na kwa vizazi vijavyo. Kwa vile CCM wana polisi, jeshi, mabomu, risasi na bunduki zote za umma wanaztumia kutunyamazisha, basi sioni kama kweli nchi hii ina mwelekeo mzuri kwani tukipinga mweleko huo tunauwawa kwa nguvu au kung'olewa meno bila ganzi!

Absolute power corrupts!
 
HKigwa was supposed to "repent" for any wrong doing he had ever committed before posting this stuff here.
Once you are in CCM you in the Ostrich Royal family; YOU BURY YOUR HEAD, SINCE YOU DO NOT SEE YOU BELIEVE YOU ARE NOT SEEN NOR DO YOU THINK OTHERS DO NOT SEE YOU.

Any one in the royal family can make any argument, but it is crocodile tears. This MP is no exception
 
Back
Top Bottom