Wachumi mko wapi????
MI nadhani haitawezaq kutokea hapa Tanzania kwa kua wakuna watu walioweza kukopa fedha kutoka kwenye taasisi za fedha za Marekani. Hii itawadhuru sana Uingereza kwa kuwa wao ndio washirika wa Wamarekani katika soko la hisa.
Ila Tanzania itaathirika kama wakileta morgage za nyumba. Hii ndio chanzo cha kuporomoka kwa soko la hisa marekani. Maporomoko yalisababishwa na hasara ambazo kampuni za nyumba (Estate dealers) walipata. Kampuni hizi zinajenga nyumba na kuuza kwa mfumo wa morgage. Hasa baada ya kupanda kwa bei ya mafuta, viwanda vingi vilikua vinapunguza wafanyakazi ili kupunguza gharama za uzalishaji. Kupungua kwa ajira kumeathiri consumption ya watu wenye kipato cha chini. Hivyo wakashindwa kulipia gharama za morgage.
Wananchi wengi walijikuta wakipoteza makazi yao (kwa kuchukuliwa na kuuzwa kwa mnada). Hata hivyo kwa kuwa kipato kilikua kimeshuka, kampuni zilijikuta zikiuza nyumba kwa bei ndogo.
Iliwapasa wananchi kuuza hisa zao ili kujikimu na gharama za maisha zilizopanda. Soko la hisa likakosa wateja.
Taarifa hizi si Rasmi, Mimi nipo Tanzania. Naomba waliopo US, watuelezee kinaga ubaga.