Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Pwani imefanya uchaguzi wa ngazi ya mkoa.Katika uchaguzi huo ambao ulifanyika Kibaha,Yusuph Kikwete ambaye ni mpwa wa Rais Jakaya Kikwete, alibwagwa vibaya na John Machemba, kwa kuambulia kura 82 tu ya kura 302 zilizopigwa.Labda wote tujiulize swali hili, kubwagwa huku kwa Yusuph kuna maana gani hasa?Kwangu mimi kuna maana moja tu,hii ni kura ya maoni kwa Kikwete binafsi na Chama cha Mapinduzi.Kama hoja za msingi ambazo wananchi zina wakera hazitatafutiwa ufumbuzi, Kikwete kushinda 2010 itakuwa kioja.Kazi kwako Kikwete.
weak point, poor argumentation! hakuna hata cha kujadili maana kila kitu ni out of point.
Nziku, polepole mzee! Out of point kwa kigezo kipi? mbona wengine wamejadili?
jumuiya ya wazazi mkoa wa pwani imefanya uchaguzi wa ngazi ya mkoa.katika uchaguzi huo ambao ulifanyika kibaha,yusuph kikwete ambaye ni mpwa wa rais jakaya kikwete, alibwagwa vibaya na john machemba, kwa kuambulia kura 82 tu ya kura 302 zilizopigwa.labda wote tujiulize swali hili, kubwagwa huku kwa yusuph kuna maana gani hasa?kwangu mimi kuna maana moja tu,hii ni kura ya maoni kwa kikwete binafsi na chama cha mapinduzi.kama hoja za msingi ambazo wananchi zina wakera hazitatafutiwa ufumbuzi, kikwete kushinda 2010 itakuwa kioja.kazi kwako kikwete.
Jamani huyo Yusuph Kikwete alikwenda kwenye uchaguzi akiwa na ajenda na sera zake, kamwe sera na ajenda zake haziwezi kuwakilisha ajenda na sera za JK. Kama umemchoka JK ni wewe lakini si vyema kumhusisha yeye JK na ndugu au uzao wake! mambo mengine naona kama yanaboa sasa! JK ahukumiwe kwa matendo yake na si matendo ya ndugu au jamaa zake au marafiki!
Mtoa hoja ana point.Ni vigumu,kwa mfano,kuzungumzia mafaniko ya kisiasa ya Ridhiwani Kikwete pasipo kumhusisha baba yake.Na kwa namna hiyo hiyo,kushindwa kwa Yusuph hakuwezi kuzungumzwa pasipo kumhusisha mpwawe,regardless ukweli kwamba uamuzi wa kugombea ulikuwa ni wa mtu binafsi.Yayumkinika kuamini kwamba laiti nyota ya JK ingekuwa inang'aa kwa nguvu miongoni mwa wapiga kura katika uchaguzi huo basi ingemsaidia mpwawe kushinda pia.Tusijifanye wagumu kuelewa kwamba chuguzi nyingi,na sio za Afrika pekee,haiba na jina la mgombea ni muhimu zaidi pengine zaidi ya sera zake.I agree na mtoa hoja,hii ni warning message kwa JK.
Kwa hiyo naye Yusufu alitaka atumie surname ya Kikwete apite? Aaa wapi, watanzania siyo wapumbavu hivyo tena.Mtoa hoja ana point.Ni vigumu,kwa mfano,kuzungumzia mafaniko ya kisiasa ya Ridhiwani Kikwete pasipo kumhusisha baba yake.Na kwa namna hiyo hiyo,kushindwa kwa Yusuph hakuwezi kuzungumzwa pasipo kumhusisha mpwawe,regardless ukweli kwamba uamuzi wa kugombea ulikuwa ni wa mtu binafsi.Yayumkinika kuamini kwamba laiti nyota ya JK ingekuwa inang'aa kwa nguvu miongoni mwa wapiga kura katika uchaguzi huo basi ingemsaidia mpwawe kushinda pia.Tusijifanye wagumu kuelewa kwamba chuguzi nyingi,na sio za Afrika pekee,haiba na jina la mgombea ni muhimu zaidi pengine zaidi ya sera zake.I agree na mtoa hoja,hii ni warning message kwa JK.